Mchumba siyo mume. Mume anawajibika kisheria na kibiblia kumtunza mke wake na watoto lakini mchumba hawajibiki kukutunza. Unapopata mchumba anayekusaidia kifedha umshukuru sana na usimchukulie kuwa ni wajibu wake. Haifai wala haipendezi kuwa unamuomba hela mchumba wako kila wakati. Ndio mnapendana sana, lakini nikuambie kitu mwanaume akiona kila siku binti unamlilia shida za hela na hamjaoana ataazimia kukuacha kimya kimya. Sio kwamba hapendi kukusaidia, ila ataona kwamba wewe unampenda sababu anakusaidia.
Hakuna asiye na shida na hela, shida zako mweleze Mungu. Mwendee Mungu kwa maombi ya kumaanisha na yeye atakuinulia msaada na kamwe usimwangalie mwanadamu kama msaada wako. Usijemkimbiza mchumba wako wakati bado mnapendana sababu kila siku beib sina salio, baby simu imeharibika nahitaji nyingine, beib mdogo wangu anahitaji ada, baby mama mgonjwa, baby nina birthday nahitaji kufanya party, beib namitumie mpesa kidogo.... hakuna walau baby nimekutumia salio, ni kuomba tu. Hapana, usijishushe hivyo wala usimuonyeshe kuwa unamuona kama mwokozi wako kiuchumi, itaku cost. God Almighty is your provider...
Source: Woman of Christ