Wednesday, July 24, 2013

Word

Ulipokuwa high school ulipanga mipango ya maisha yako kuwa utaenda chuo, utapata kazi then utaolewa na kuwa na familia yako. Ukaweka kwenye maombi na bidii ya kusoma na kumtumikia Mungu.
Ukamaliza chuo kwa ushindi, ukapata kazi nzuri na hadi vyeo umepandishwa, unamtumikia Mungu kanisani... Lakini huna amani, unaona umri umekwenda nawe hujaolewa bado. 

Kwako hili limekuwa jaribu kubwa sana. Unaona kama Mungu amekuacha, amekusahau na hakupendi. Shetani anatumia mwanya huu kukudanganya utafute mtu uzae naye maana umri umekwenda. Napenda kukutia moyo kuwa usikate tamaa, angalia mengi ambayo Mungu amekuvusha, hata hili halo litapita. Usikubali kumkosea Mungu kwa sababu ya jaribu lako. Mungu hasinzii wala halali usingizi, anajua hitaji lako na anasikia kilio chako na kwa wakati wake atakujibu na kila mtu atashangaa.


Source: Woman of Christ

Reactions: