Monday, June 24, 2013

Wababa mpo????


Leo nataka kuongea na wababa. Wanawake wengi wamekuwa stressed sana baada ya kujifungua na kujikuta wamebadilika maumbo yao hasa tumbo na kunenepa. Wanawake hawa hujitahidi kwakweli kufunga tumbo na njia nyingi ili kurudia hali ya kawaida. Miili haifanani, wengine hufikia hivyo mapema kuliko wengine, wengine huwa ni ngumu sana sana na wengine huamua kutonyonyesha kabisa ili wasile. Kumbuka tumbo la mama huyu limestrech slowly for nine months. Na mwili umeongezeka kidogo kidogo kwa muda mrefu, hivyo huwezi tarajia arudie hali yake overnight.

Tatizo ndio huanzia hapa. Utakuta mume anaanza kumsimanga mkewe "angalia ulivyojinenepea, tumbo baya limejaa michirizi, mbona fulani karudia hali yake, n.k n.k", jamani miili haifanani, hilo tumbo unaloona limejaa michirizi ni sababu watoto wako uwapendao sana walitafuta hifadhi huko. Sisemi wanawake tusirudie hali za mwanzo, la, ila mume usimsimange mkeo sababu ya mabadiliko ya mwili sababu ya uzazi. Pamoja mtafute njia za kumsaidia, mnaweza ruka kamba pamoja, situps mkafanya pamoja na mazoezi mengine. Wengi wetu muda wa kwenda gym au kukimbia haupo, ila pamoja mnaweza kusaidiana.

Diet husaidia sana, ila diet sio kazi rahisi. Wewe mume unataka mke akupikie mapochopocho ila yeye aishie kula mboga na matunda, Inawezekana kweli??? Fanya naye diet kuonyesha ushirikiano. Kumsimanga sababu ya unene au ukubwa wa tumbo hakumsaidii zaidi kutampa stress ambazo zitamfanya azidi kula. Hivi ni wanaume wangapi wamewahi kufanya diet??? Diet sio lelemama, hivyo msupport na sio kumsimanga. Tena ukiangalia hao wanaowasimanga wake zao wao ni wanene na wanavitambi ila wake zao hawawasimangi. Leo unamchukia sababu amenenepa, je umewahi waza itajuwaje akikatwa ziwa?? Na akipata fistula je?? Mtu kakuletea watoto wazuri kwa uchungu mkubwa na mara nyingine operation, kachungulia kaburi, shukrani yako inakuwa kumsimanga???


Source:Women of Christ