Monday, June 24, 2013

Kama sio lako la jirani yako....


Wasichana wapendwa... Mwanaume hakamatiki kwa kumpa mwili wako auchezee. Mwanaume hakamatiki kwa kushika mimba yake.
Mwanaume hakamatiki kwa kumpikia na kumfulia.
Mwanaume hakamatiki kwa kuacha kifua na mapaja wazi.
Mwanaume hakamatiki kwa makeup zilizopitiliza.
Mwanaume hakamatiki kwa kumnunulia gari na kumpa fedha za matumizi.

Hayo yote hayawezi kukufanya umpate mume, au umkamate mwanaume, zaidi yatakuletea maumivu ya moyo...

Wewe ni wa thamani sana, ni ua, haupaswi kukimbiza kipepeo bali vipepeo ndio wakutafute hadi wakupate. Kipepeo haendi kwenye ua lisilo na harufu ya kuvutia. 

Harufu ya tabia njema na bidii ya kazi.
Harufu ya kumpenda na kumcha Mungu.
Harufu ya kujiamini, kujithamini na kujiheshimu.
Harufu ya kuwajali wengine na ukarimu.
Harufu ya usafi wa moyo, maneno, tabia na mwonekano wa nje.

Hakuna haja ya kutafuta kumkamata mwanaume, kwa harufu hizi za kuvutia mwenyewe atajikamata kwako.

Source:Women of Christ

Reactions: