Monday, June 24, 2013

KWENU WANAUME WENZANGU TENA....Nimeitoa sehemu

Umemdanganya mtoto wa watu unampenda, akakuamini, akasahau hadi tarehe akaona zote ni February 32.
Umempa mimba mtoto wa watu mzuri tu, amehenyeka na mimba miezi 9 amekuzalia mtoto..
Ghafla umemtelekeza eti huna plan nae, eti sio chaguo lako, eti mimba ni bahati mbaya tu hukupanga...
Uongo mtupu na ghiliba za nyani mzee. Ulivyokuwa unapewa tunda
bure, unakatika kwa spidi kama umefungwa injini ya boti ya Horsepower 6 ulitegemea nini?

Mbona wanaume tunakuwa migumegume hivi lakini?
Mtoto wako mwenyewe hata hujui anakula nini, anavaa nini.......kweli?
Unatanua na mademu wengine
mwanao hujui anaumwa, katibiwaje, kapona au lah kweli?

Mngefungwa uterus japo mkae na mimba wiki 3 kama panya mngejifunza kuacha upuuzi huu.
LEA DAMU YAKO,we si kidume?
Wanaume wa dizaini hii ni aibu kwa taifa. Ukijifanya Fundi wa kukatika kama Fally Ipupa uwe pia fundi wa kulea!

Ukichukia Poa tu lakini mi nimemaliza.