Friday, June 28, 2013

Siku ndio hizoooooooo....

Jamani mashoga zangu jumapili ijayo ndio 7/7/2013 siku yetu ya mafundo kwa wanawake kwa ujumla na haswa kwa wale wanaotegemea siku moja kuingia kwenye ndoa, wale wenye wachumba na wale ambao wapo kwenye ndoa kwa ujumla ni mwanamke yeyote 18+..

Ndio ushakuwa mkubwa hapo unautambua mwili wako na mabadiliko na unatambua mwili wa mwenza wako au mumeo vyema, sasa basi labda hujawahi kufundwa wewe ndio utafundwa siku hiyo kwanzia kwenye chakula shoga inahusu nini mwanaume wako aende mzunguko mmoja au miwili au kwa mwezi asiende kabisa eti anakwambia amechoka, shoga kweli inawezekana amechoka lakini wewe kama mkewe/kama mpenzi wake unajuwa chakula gani uumpe umboost nguvu..hahaha halooo hujui shoga ndio uje tukujuze.

Shoga hapo nimekupelekea jikoni shoga yangu sasa nakurudisha chumbani unapolala na mpenzi wako shoga kitanda chako unakimudu, pinde zake unazijuwa, na masharti yake je au wewe ndio ilimradi kitanda basi unakilalia tu hata kwa kujitupa..halooo wenzio tuliofundwa tukikuona tutakucheka.

Hichohicho kitanda anapolala mpenzi wako unamfanyaje unajuwa kumsinga, unajuwa kumpa raha unajuwa kutumia mikono yako au wewe shoga yangu ukilala tena ndio umelalaa mgongo mgongo na wewe kama mgonjwa unadripu tena bora hata mwenye dripu anaweza kulala ubavu wewe hata ubavu huwezi...haalooo shoga sitaki kukumalizia uhondo ukija utaona.

Shoga mwanaume anataka malezi kama mtoto mchanga, inahusu nini ukaolewe leo mwaka uachike hukufundwa wewe bibi mwanaume ndio kichwa cha familia wewe mke ni shingo unauwezo wa kukigeuza kichwa utakavyo tutakufunda kukigeuza kwa maringo tena kwa ujuzi ma maubunifu kibao shoga siye tunajuwa kuolewa tu kuachika hatujui...

Shoga nyonga kila mtu anayo ni ujuzi wako wanaume siku hizi wapo kitandani wanaokata nyonga sasa wewe umelala tu mkavu kama umeona mzimu inahusu...njoo uone wanawake wenye nyonga zao

Shoga bafuni je unalijuwa bafu lako unalitumiaje na mpenzi wako, bibi wee haijalishi kama nyumba ya kupanga au umejenga shoga utafundwa bafu lina raha yake, bafu lina masharti yake ukiwa na mwanamme bibi wee nisikumalizie uhondo uje usikie mwenyewe...

Tukutane siku hiyo lipia ticket yako mapema zimebaki chache tunataka watu 100-150 tu hatutaki wengi hatutaki vurugu kila mtu afundwe aelewe aweze kuuliza maswali kwa uhuru, lakini kwa wale mnaoogopa tutawapa vikaratasi muandike swali tutayasoma...kupata tickets nipigie 0717 019320 kwanzia watu watatu tunakuletea ulipo kwa ambao hawawezi kuja kuchukuwa tickets na mnataka kuja mnaweza kutuma hela kwenye tigo pesa tutaandika jina lako ticket yako utaikuta mlangoni siku hiyo na mkumbuke ni kwanzia saa tano asubuhi mpaka kumi na mbili jioni shoga ili usiku ukampe mzee maraha uliyofundishwa...halooooo

Haloooooo ikipita hii MUNGU akipenda tutakutana tena mwezi wa kumi na mbili kama tutakuwa hai....

Reactions: