Thursday, June 27, 2013

Mwanamke kufundwa bwana...

HUKU siku za kufunga ndoa zikihesabika, mkongwe kwenye filamu za Kibongo, Suzan Lewis ‘Natasha’ amefanyiwa sherehe ya kufundwa kabla ya kwenda kwa mumewe ambayo huko mitaani inajulikana zaidi kwa jina la singo.

Shughuli hiyo ilifanyika mwishoni mwa wiki iliyopita, Tandika Maghorofani, Dar ambapo iliandaliwa na shostito wa Natasha aliyejulikana kwa jina moja la Nuru.
APEWA SOMO
Natasha aliwekwa ndani kwa muda wa saa moja akipewa somo la ndoa na watu maalumu walioandaliwa kwa ajili ya shughuli hiyo kabla ya kutoka nje kuungana na wageni waalikwa.


  Alipotoka nje, alikutana na waalikwa ambapo kati yao ni mastaa mbalimbali Bongo kisha wakaungana kwenye zoezi zima la kucheza ngoma.
KIASILI ZAIDI
Waalikwa walipata nafasi ya kupakwa urembo mbalimbali wa kiasili usoni na kuifanya hafla hiyo iwe ya kipekee kutokana na vivutio hivyo. 
Baada ya yote hayo kukamilika, msafara wa kuelekea nyumbani kwa Natasha, Yombo ulianza huku ngoma zikiendelea kupigwa na mastaa mbalimbali wakikata mauno ndani ya gari.

Akizungumzia shughuli hiyo, Natasha alisema: “Nashukuru sana jamani kwa kupita hatua hii ya kwanza kuelekea kwenye ndoa yangu. Siwezi kuacha kumshukuru zaidi rafiki yangu Nuru kwa kunifanikishia.”

Source: Global Publishers