Wednesday, June 12, 2013

Gharama za harusi kwetu hakunaga...

WANANDOA Charles Kanyema (29) na Bi. Onoratha Pascal (28) hivi karubuni waliwashangaza wakazi wa Manispaa ya Morogoro baada ya kwenda kufunga ndoa wakiwa wamepanda bodaboda na kurejea nyumbani kwa kutembea kwa miguu.
Ndoa hiyo iliyofungwa katika Kanisa Katoliki Jimbo la Morogoro Mjini na kufungishwa na Paroko Msaidizi, Padri Phidelisi Mwesongo iligharimu shilingi 45,000 tu.
“Gharama hizo ni pamoja na picha 5 kwa ajili ya kumbukumbu yetu na  nyumbani tumenunua mchele na nyama kwa ajili ya  sherehe ndogo,” alisema bwana harusi Kanyema.
Alisema fedha hizo zilitokana na michango waliyochangiwa na wana jumuiya wenzao na hawakutaka mambo makubwa katika sherehe yao.
Mara baada ya kuwafungisha ndoa, Padri Mwesongo aliwataka wanandoa hao kutambua kwamba maisha ya ndoa ni magumu na yanahitaji uvumilivu ili ndoa yao iweze kudumu.
Baadhi ya watu waliohudhuria sherehe hiyo waliwasifu wanandoa hao kwa kutotumia gharama kubwa wakidai kwamba mara nyingi ndoa zilizojaa kila aina ya mbwembwe huwa hazidumu.

Source:Global Publishers

Reactions:

0 comments:

Post a Comment