Wednesday, June 12, 2013

MUNGU wangu kweli baba nanihiiiiiiiiiiiii........

Tukio hilo lilishuhudiwa na watu kibao, lilijiri Juni 10, mwaka huu katika nyumba moja ya kulala wageni iliyopo Kinondoni jijini Dar.
Kunaswa kwa wanaume hao ambao ilidaiwa walikuwa kwenye harakati za kufanya Usodoma na Ugomora, kulifuatia mke wa mmoja wao kunasa meseji za kimapenzi walizokuwa wakitumiana wawili hao.
Mama huyo alipobaini meseji hizo chafu, wawili hao wakisisitiziana kukutana kwenye gesti hiyo usiku wa siku hiyo, alimpigia simu mmoja wa waandishi wa Global ambapo mazungumzo yao yalikuwa kama ifuatavyo:
Mwanamke: Haloo haloo! Nazungumza na mwandishi wa Global?
 Mwandishi: Ndiyo, dada tukusaidie nini?
Mwanamke: Naomba msaada wenu jamani, nataka kumfumania mume wangu ana tabia chafu sana!
Mwandishi: Tabia gani?
Mwanamke: Anafanya vitendo vya kishoga na leo amepanga kukutana na huyo mwanaume mwenzake gesti (akiitaja) iliyopo Kinondoni, nimeona meseji walizokuwa wakichati.
Mwandishi: Unaweza kuja ofisini kwetu ili tupange namna ya kuwafumania?
Mwanamke: Si hapo Bamaga?
Mwandishi: Naam.
Mwanamke: Kwa kuwa nipo mitaa hii ya Kijitonyama nakuja sasa hivi.
Baada ya nusu saa mama huyo alitinga Makao Makuu ya Global, Bamaga-Mwenge na kuweka kila kitu wazi ambapo kikosi kazi kilijiandaa kwa ajili ya kazi hiyo.

FUMANIZI
Ilipofika saa 1:30 usiku, timu yetu, mama huyo, wapambe wake na polisi walikuwa wanafanya doria nje ya gesti hiyo.
WANAUME WATINGA GESTI
Saa 5:30 usiku, mume wa mwanamke huyo akiwa na mwanaume anayedaiwa kuwa shoga walifika gesti hiyo bila kujua kama waliwekewa mtego wa kunaswa na kwenda kuchukua chumba namba 2.
Wakiwa ndani, mke alimpigia simu mumewe na kuhoji alipokuwa akajibiwa alikuwa mitaa ya nyumbani kwao Manseze, Dar akipiga stori na rafiki zake.

MKE, POLISI, WAANDISHI WATINGA NDANI
Wawili hao wakiwa wanajiandaa na mchezo wao usiofaa, polisi aligonga mlango akijifanya mhudumu aliyetaka kumpatia taulo, jamaa bila kujua alifungua ndipo walipofumaniwa na kuibua varangati zito.
Kufuatia timbwili hilo, waliwekwa chini ya ulinzi na kutolewa pale gesti tayari kupelekwa kituoni ndipo mwanaume anayedaiwa kuwa shoga akatimbua mbio mithili ya mwanariadha wa kimataifa, Usain Bolt wa Jamaika na wanandoa hao waliendelea kuzozana huku mke akimlalamikia mumewe na kumwambia wakifika nyumbani ampe talaka yake.
Hata hivyo, mwanamke huyo aliomba sakata hilo lisipelekwe polisi kwa madai alichotaka ni kumfumania mumewe na kwamba alikuwa na ushahidi wote.

Source: Global Publishers...kweli hapana chezea nyie

Reactions:

0 comments:

Post a Comment