Habari toka IFM - Dar es salaam ni kwamba mwanafunzi mmoja ambaye bado hatujafanikiwa kulipata jina lake amefariki dunia kwa kulishwa sumu katika chakula alicholetewa na mpenzi wake ambaye ni mke wa mtu.
Taarifa zaidi zinadai kwamba Mwanafunzi huyo alikuwa na uhusiano wa karibu sana na mke wa mtu ambaye mbali na starehe za kimapenzi alikuwa pia anampelekea chakula cha jioni baada ya mchezo huo kudumu kwa muda, mume wa mwanamke aliusoma mchezo mzima na kuandaa Mtego wa kuwaangamiza wote.
Habari zinadai kwamba siku ya jumatano jioni mwanaume huyo aliwahi kurudi nyumbani na kufanikiwa kukinasa chakula kilichokuwa kimeandaliwa tayari kwa kupelekwa kwa huyo mwanafunzi ambaye alikuwa anatembea na mke wake.
Baada ya kukinasa, alijifanya kuzuga na kupotezea. Mkewe alipotoka alikichukua na kukitia sumu chakula hicho na kisha kukiweka kama kilivyokuwa kimeandaliwa.
Lengo lake lilikuwa ni kuwamaliza wote maana alijua ni lazima akifika watakaa na kula pamoja.
Mwanamke alipopeleka chakula hakukaa kula na badala yake alimwambia yule mwanafunzi kuwa mume wake amewahi kurudi siku hiyo hivyo hatoweza kukaa wale pamoja. Mwanafunzi huyo akakipokea na kukila na ndipo mauti yakamkuta.
Habari toka chuoni hapo zinadai kwamba mwanafunzi huyo alikuwa amesha disco lakini alikuwa
amepewa nafasi nyingine ya kurudia mwaka wa pili , hivyo aliendelea kukaa mtaani kama mwanafunzi.
Mwili wa marehemu bado uko Muhimbili kwauchunguzi zaidi baada ya polisi kuuzuia kuzikwa.
Hizi ni habari mbaya sana kwa wanafunzi wa chuo hicho maana ni jumatatu tu mwanafunzi mwingine alifariki katika hali ya kutatanisha baada ya kifo cha mpenzi wake miezi michache iliyopita.
Habari za ndani zaidi zinadai kuwa toka mwaka huu uanze mpaka sasa chuo cha IFM kimepoteza
wanafunzi 12 huku wawili wakiripotiwa kuwa na hali mbaya zaidi katika hospitali ya Muhimbili.
Source: Flora Mbasha
So sad kwakweli..i know him.
ReplyDeleteNA HUYO MWANAMKE HATOSHELZWI NA MUMEWE AU NI NN?
ReplyDeletehuyo mwanamke amezoea miti mingi
ReplyDeleteAsingefanya fanya hivyo hata kama amekosewa. Je na wengine wangekula maskini?maisha ya uanafunzi msosi wa home kila mtu anautamani. Huyo mtu hana ubinadamu. Mkewe ndio alikua tatizo alilotakiwa kudili nalo na si huyo kijana
ReplyDeleteUzinzi utatuua watanzania. Ni vyema tukarejea kwa Mungu kwa Kuacha Uzinzi!
ReplyDelete