Monday, May 20, 2013

Mabig...ndoa hizi

wanaume za watu nao wamezidi kutongoza tongoza kuliko ht single boys.nina rafiki yangu yaani yeye alitongozwa bila kujua km yule mwanaume ni mume wa mtu.
Ni mwaka wa pili sasa yuko nae,amempangia na gari kamnunulia na amemuajiri kwenye kampuni yake.kila siku anampitia bidada wanaenda wote kazin,jion wakitoka anaenda kwa bidada anakaa hadi saa sita ndo anaondoka.akisafiri wako wote,yaani asilimia 95 ya mda wa mwanaume yupo na bidada.sasa kumbe kijana ana mke na amezaa nae watoto watatu.

Na mwanaume huwa anaenda na huyo dada tanga kwa wazazi na ndugu zake mara nyingi.na hamna aliemwambia kuwa kijana kaoa.zaidi wanampokea kwa nderemo na vifijo.
 
Na mwanaume alimbembeleza bidada azae nae angalau mtoto mmoja.mwanaume ni mkristo na kumbe alifunga ndoa kanisani.sasa bidada ana mimba ya miezi mitano.na mwanaume mapenzi ni moto moto.

Sasa jana kuna mfanyakazi mmoja kwenye kampuni ambayo ni ya huyo mwanaume akamwambia bidada ukweli kuwa kijana ana mke na mwanae wa kwanza ana miaka mitano.wa mwisho miezI tisa.kumbuka dada anafanya kazi kwenye kampuni ya kijana.
bidada akaamua kumuuliza kIjana maana hakuamini, walivyotoka kazini jana wakapitia mahali kula akamuulizakijana akakubali ni kweli akamtajia na majina ya watoto akamuuliza mbona hajamwambia siku zote akamwambia kila jambo na wakati wake wakati wa kukwambia ulikuwa haujafika nilijua utaumia na mimi sipendi uumie akaomba sana msamaha kwa kumficha siku zote hizo.
Bidada akamwambia nahitaji msimamo wako akamwambia nawapenda wote mke wangu tumejenga nae nyumba ndo tiunayoishi,ndo maana na wewe nakujengea.mke wangu nimemnunulia rav 4 nyekundu wewe ya silver.mke wangu anastationary kubwa ya kutengeneza macounter ndio mana na wewe nimekwambia uchague biashara maana haya maisha kuna leo na kesho.nyie wote ni wake zangu ndo mana mda wote wa mchana niko na wewe na yule usiku.sitaki kumuacha hata mmoja bi dada akachannganyikiwa hajui afanyaje.

Anaomba ushauri

Reactions:

9 comments:

 1. hii noma kudadadeki..na huyo mkewe kila siku mwanaume anamrudia juu ya saa sita amekaa tu kimya..kweli huyo malaika na amefundwa haswa..

  mimi naona atulie kwanza asimuache jamaa kwakuwa tayari ana mimba na mtoto anahaki zote za kulelewa na baba na mama ila tu nyumba ikishaisha na biashara kapata shoga aende amatafute mke wa jamaa amueleze ukweli ajuwe kwamba wapo wawili ni ngumu lakini hapo atajuwa kama kweli jamaa anampenda hatokana mbele ya mkewe na mkewe atajuwa anamke mwenzie nje watajuwa jinsi ya kuishi kwakuwa kuna leo na kesho na watoto ni ndugu baadae watahitajiana

  kwani si kuna wanaume wameoa wake zaidi ya mmoja na kila mtu ananyumba yake na maisha yake sasa je..hapo hakuna kuachia mwanzo mwisho..na ahakikishe ameenda kutubu kwa MUNGU wake kwa kuingilia ndoa ya watu japo hakujuwa

  maandiko yanasemaje mwanamke aliumbwa kutokana na ubavu wa mwanamme siamini kama ubavu mmoja ulitoa wanawake wawili..ila muombe sana MUNGU akuongoze katika hayo maisha.maana kama aliweza kufanya hivyo na wewe asije akatafuta na mke wa tatu akaendeleza gurudumu..

  ReplyDelete
 2. mh hatarii jamani

  ReplyDelete
 3. hapo Rose sijakupata mama leo unanichanganya, ingekuwa wewe Rose ndio huyo mwanamke alizaliwa huko nje ungefanyaje, pls reply

  ReplyDelete
 4. au sababu rafiki yako ndio kachukua mume wa mtu??

  ReplyDelete
 5. wakati huyo bwana anaenda kwa huyo bibie na kuondoka saa sita usiku kila siku ilikuwa makubaliano au nini, huyo dada alikuwa anajua anatembea na mume wa mtu, usitudanganye Rose please, hii story haijatulia naona.

  ReplyDelete
 6. Jamani hii strory mimi mwenyewe nimeandikiwa nikaipost humu apewe ushauri sasa nifanyaje hapo nimecopy na kupaste labda kama aliyenitumia nimuongo mwenyewe atakuwa anajuwa maana anaingiaga humu..nataka niwaambie humu hizi story ninazoweka humu ni true story za watu ndio maana niko tayari nisipost kitu hata week mbili kama sina story..hakuna vya kutunga humu..na nilivyomshauri kufanya ndio mimi ningefanya hivyo hata ingekuwa imenitokea mimi, huyo mtoto yeye anakosa gani asipate malezi ya baba na mama kisa ujinga wa baba yake inahusu..ndio maana nikasema inauma sana lakini lazima mke afanye maamuzi kulingana na haki sio kulingana na moyo unasemaje..ndoa sio mchezo wa kuigiza jamani, ni maisha ya kuishi kwa hekima na busara sio uone tu sifa kutembea na pete zako barabarani..

  Ahsante

  ReplyDelete
 7. Hahaha umenichekesha eti au sababu rafiki yako kachukuwa mume wa mtu...wala huwezi amini wala simjui huyo dada amenitumia tu email halafu kwanza mimi hata marafiki zangu wananijuwa huwa sina marafiki wanaochukuwa wame za watu kwasababu hiyo huwa nawapinga sana na kuwakataza sana na sipendi na hata kama wanafanya basi hawajawahi kunihadithia na wala sitaki kuwauliza..

  Mimi kazi yangu ni kuwa pamoja na wanandoa na kueleweshana na kusaidiana matatizo ya ndoa sasa natakiwa kuwa mfano kwao kwanini tena niwachekee marafiki zangu wanaochukuwa wame za watu..hakunaga kitu kama hicho kwangu

  ReplyDelete
 8. duuu ila ni ngumu cause, unajua once uko na mumeo kuna mipangilio mingi ya maisha mnapanga, iwe hivi iwe vile, leo another woman with mtoto na cost ya kijengewa house, mmmmmh ngumu kumeza ukiwa mdada mwenye ndoa kwa kweli, inauma sana hawa wanaume jamani,

  ReplyDelete
 9. Mradi na ni uzembe kwa nini?? Nae hamchunguzi mume wake anatokea asojua kumdadisi mumewe

  ReplyDelete