Thursday, May 23, 2013

Mabig...ndoa hizi part 2:

Basi jumatatu akaondoka baada ya ushauri akarudi kwake.jion mwanaume alivyotoka kazin km kawaida yake akaja kwa bidada kumuangalia maana alimdanganya anaumwa.
akamlazimisha hadi akampeleka hosp.kucheki malaria bidada akawa na mdudu mmoja akamchukulia dawa wakarudi kwa bidada.kwa vile mdada bado alikuwa anatafakari akawa hana furaha.mwanaume akawa anajitahd kumchangamsha changamsha akiamini mdada anaumwa
kijana hajaondoka hadi asubuhi.asubuh ilipofika akaenda kazini akarudi mchana.ili wadiscuss hyo issue maana mdada alimwambia ana maongezi nae.akamwambia ya prisca ofisi hakukalik nataka kujua una mazungumzo gani ila nakuomba twende b'myo tutafute hotel nzuri tulale hadi kesho ndo tutaenda kuongelea huko naamini kila kitu kitakua poa mdada akakubali akajiandaa wakaenda kwenye saa nane hv hapo ilikuwa jumanne.
kufika huko mwanaume kaomba hadi kalia.hataki waachane.hadi kawa km amechanganyikiwa.na bidada akamwambia ndoto zangu ilikuwa nije niwe na mume hvyo umeniharibia maisha kijana akamwambia ameshajua cha kufanya hvyo bidada awe na amani wakalala.
sasa leo jumatano wakatoka bmoyo akamrudisha mdada home yeye akaenda kwa ofisi
kama saa saba akarudi na wazo kua hataki mdada ateseke hvyo ameamua kumuacha mke wake rasmi ili abaki na bidada kwa madai alikuwa anaishi nae kwa ajili ya watoto na anaona hao wawili wamekua wakubwa atawapeleka boarding huyo wa miez tisa atamchukua akifika miaka miaka 3 wakabishabana maana mdada anaona huruma kwa mke mkubwa japo nae anampenda jamaa.
kijana kasema anamwachia mkewe kila kitu coz hataki kumuumiza.nyumba na stationery anayomiliki mkewe hatavigusa.
sasa kilichonifanya nimalizie huu umbea ni jamaa kaja jion kwenye saa nne kabeba bag kubwa km mbili eti wakae hapo kwa bidada kwa mda huku wanatafuta nyumba nzima wapange.ndo bidada haelewi maana anampenda na anaonea huruma familia yake.amechanganyikiwa maana atakua km ameolewa na kwao wanajua ana mimba ila wanajua anaishi mwenyewe.

Bado tunataka kujuwa wapenzi hawa wataendeleaje..nitawaletea tena hii story maana nimeambiwa nitatumiwa tena...

MMhhh wanaume hawa!!!! unaambiwa tumekutana kimjinimjini na siku tutaachana kimjinimjini


Reactions:

2 comments:

  1. Umenigusa sana mleta stori ,kwan hata mie yamenikuta kama ya huyo dada,jaman yackien tu kwa watu dunia hii wa kumuamin n Mungu pekee.

    ReplyDelete
  2. MMMMMHHHHH aliyotendewa mwanamke mwenzetu na mumewe sijapenda. na huyo bibiye ajue kabisa whats goes around comes..... sijui lakini ila sifagilii hata kidogo mwanaume kumwacha mkewe huyo dada awe makini sana. kama huruma kwa mwanamke mwenzie anayo kweli, she has to think twice, lazima yamkute makubwa kuliko ya mke wa kwanza.

    ReplyDelete