Wednesday, May 22, 2013

Inasikitisha sana...Part 1

 kuna rafiki zangu, walioana, baada ya miezi kadhaa wakapata mtoto, but wakati wanapanga mpango wa kuoana, hawakupima afya zao kama ilivyo siku hizi, kwa sbabu they use to be "Lovers" for so long, binti akiwa form two, kaka akiwa form five, in the same school, so they didn't see the importance of being screened. Alipojifungua huyu shosti angu, mtoto alikuwa 'mnyafu nyafu', yani hakuwa na fanya nzuri, nakumbuka alizaliwa February 28, akafa February 29, mwaka uliofatia, tukaenda kuzika mkoani,but dalili za mtoto zikaonyesha kwamba alizaliwa ameathirika, baada ya msiba rafiki zangu wakashauriwa kwenda kupima, wakaonekana 'wameathirika'. Wakajihoji sna hii imetokea wapi? mbona tumekuwa waaminifu sna tangu tuko shuleni? Ndipo yule bwana akakumbuka jinsi alivyouguza familia ya baba yake mdogo kule mkoani, alivyoshambuliwa na ukimwi, sasa kwa kuwa ni enzi zile, hawakujua kama ni UKIMWI, wakasema hapana hii familia " IMELOGWA" kwa kuwa baba ni mbunge, kwa hiyo "wamewaonea wivu". walisema hivyo kwa kuwa waliugua familia nzima kwa wakati mmoja na kufa, unaambiwaa ukienda kijini kwao kule nani hii, makaburi yamejipanga kwa kufuatana!


Huyu baba mwenye nyumba alikuwa ni mbunge, mkewe akamwambia huko Dodoma mnakaa muda mrefu sna wakati wa Bunge, hebu tafuta wenyeji huko, wakutafutie msichana wa kazi, maana wa hapa mjini, sio watulivu. haya, kweli baba akafanya vile. Akaomba wenyeji wamtafutie housegelo, akapata binti wa Kirangi, mweupe pee, yaani "mwali mbichi " ng'ari ng'ar. Kumbe yule binti ni mwathirika, akasafirishwa na mh. Mbunge mpaka kwao Mbeya, akaanza kazi za ndani pale. Sasa basi, watoto wa kiume wa yule mbunge ni wakubwa, wanasoma secondary, wengine vyuo, wakija likizo, "wanapumzika kwa dada", baba yao naye, anapumzika hapo, baba wadogo wanaokaa pale nao wanajipumzisha pale, dereva wa yule mbunge naye anapumzika na mke wa mbunge yule, unaona chain hiyo? sasa muuguzaji wa ile familia akawa ndo huyu mume wa rafiki yangu, maskini, mtoto watu hakuna cha kuvaa gloves wala nini, umetoka kijijini umekuja pale kusomeshwa, inabidi uwe mtii tu, kuwaogesha kuwanawisha n.k, ndipo alipopata huu ugonjwa.

Wale wandugu walianza kufa kwa kupishana wiki tatu, mwezi, mpaka wote wakafa! Na dereva yule naye akafa na na mkewe huko alikokuwa. Kwa hiyo vitu kama hivi wandugu tusivipuuzie, usiseme mie sina watoto, kumbe una wadogo zako pale, shemeji zao, n.k! MWenye masikio na asikie!

Sasa kesho tutaangalia na screening ya kiroho pia, hii ni kwa wale mahouse gelo wachawi. Ndugu zanguni,this wolrd is not a bed of roses, ni uwanja wa vita, tumezungukwa na mambo mengi sana ya nguvu giza. Niliombwa na wifi wa mdogo wangu kumsaidia kumpokelea house girl wake stand ya mkoa pale Ubungo na kumpeleka kwake kwakuwa alikuwa na shughuli fulani akashindwa, kufika pale nyumbani, cha kwanza alichofanya ni kumsalimia house gelo na kumwambia kwamba wao ni watu gani na imani yao ni nini, na kwamba "lazima tukuombee' kwanza ndio uingie chumbani ukaoge na kuweka virago vyako, nilimwona huyu wifi sasa analeta "unyanyapaa wa kiimani" kumbe she knew what she was doing! Yalishamkuta ya kumkuta! Can you guess what Happened while praying for that house maid?Kesho tutaendelea.

Stella

Reactions:

1 comments:

  1. mmh jaman kwel dunia imekwisha twashukuru kwa kutufahamisha mumie ila unakatiza utamuu

    ReplyDelete