Thursday, May 23, 2013

Inasikitisha sana...part 2

asa yule binti tuliyeishia story yake jana, baada ya kufika pale na kuombewa, ndugu , yalipanda mapepo hayo, tena bora pepo, sasa hili lilikuwa ni JINI MAHABA, mpo hapo? likaelezea weeee, na mwishowe ikabidi tu kusalimu amri na kuondoka, ndo yule binti kufunguliwa na kuanza kujielezea kwamba ni kweli huwa anateswa na majini. sasa wandugu, hili jini pale nyumbani mnadhani lisingeleta madhara yoyote? uharibifu, mafarakano, n.k?


Zifuatazo ha simulizi halisi ambazo nimeziona mie mwenyewe kwa macho!

Kuna mama fulani pale mjini kati, alipata housegelo, kumbe yule binti alikuwa ni mchawi, alikuwa anajigawa mara mbili katika kufanyakzi zake, nyumba ile ni ya ghorofa, pale upanga, kwa hiyo at the same time, yuko jikoni anapika na yupo bafuni anafua, mpo hapo?
Kuna mwingine huyu ni shangazi wa staff mwenzangu, yeye alipata binti wa hivyo pia, huyu sasa alikua akienda kuwanga usiku na ungo, anaondoka na mtoto wa boss wake mdogo, anambeba mgongoni na kupaa naye, ili tu asilie huku chumbani wakati yeye akitoka, kwa hiyo anaamua kuruka, naye, afya ya huyu mtoto ilikuwa mbaya sna kwa sababu ya baridi, na mbu waliokuwa wanamuuma kila siku.

Kuna huyu mwingine hapo Kibangu kwa shosti yangu vile vile, halafu wamama haya mambo ya kutuma tu nauli uletewe binti kama unaagiza vocha dukani haipendezi! jirani yake alikuwa anaenda kwao mahenge likizo, akampa nauli kwamba amletee housegelo, without knowing kwamba huyu jirani yake "si mwema", kurudi akaja kweli na binti, kumbe walikuja na ungo, sasa kuna kosa alifanya kwenye hii familia ya shoti wangu, akachukua Ubongo wa mtoto wa shosti, kwa hiyo yule mtoto akawa taahira ghafla, yaani zezeta kabisa kwa kutoa udenda, nafupisha tu kwamba, baada ya kumuomba Mungu kwa muda mrefu, binti mwenyewe akakiri kwamba ni yeye ndo amemfanya Joshua kuwa zezeta, aliagizwa na mama wa jirani wamle nyama, wakashindwa kwa sababu wazazi "wanasali sana', wakaamua kumfanya zezeta ili kuwakomoa, sasa basi walipoamua kumrudisha kwao, ndo akasema mie siwezi kurudi na bus, kwani mlikujaje? tulikua na ungo! mpo hapo? ndo huyu shosti wangu kujua kwamba kumbe jirani yake alikuwa ni wa ulimwengu ule wa kule "chini'.

Sasa basi it happened, shosti yangu fulani akawa naye anashida sana ya msichana wa kazi maana ana mtoto mdogo, nikamshauri amwombe Mungu while anatafuta na sio akurupuke tu kutuma nauli mikoani, si nikaanza kumweleze hii stiry ya hapo juu? Without knowing kumbe kwa simulizi ile, ni Mungu alikuwa anamfungua macho ili ajue binti yake anayetaka kumwondoa yukoje! my darling friends, unaweza kuona hizi ni story tu hazikujengi wewe, kumbe ikawa ni namna fulani Mungu anaitumia kusema na mtu fulani humu ndani!

Guess what? Kesho yake anatoka kazini (alikuwa ni daktari wa Police oysterbay), kwa hiyo saa kumi anafika nyumbani, akakuta binti anapoza uji ampe mtoto wake, mhh! akasikia sauti moyoni inamwambia, hebu muulize binti ameweka nini kwenye uji wa mtoto? hakupingana na ile sauti, authoritatively, akamwuliza dada, umeweka nini kwenye uji? mhh! hapo ndipo mziki ulianza, mind you ni jana tu nilitoka kumpa story ya huyo binti wa Kibangu aliyemloga Joshua, mtoto wa shosti yangu. Hee, binti si akasema nimeweka " dawa", kuulizwa dawa gani kwani mtoto anaumwa? Mind you ni daktari huyo mama, binti akajibu, kwani mama hujui kama mimi ni mchawi? Mhh! shosti wangu akatoa macho , akaanza kuuliza vingine alivyofanya mle kwenye ile familia, wandugu binti akasema, huwa nawawekea bafuni maji ya kuoga ya maiti, unayapata wapi, akasema mama wa nyumba ya pili ana kisima chake kule uani kwake, kwa hiyo huwa ananipa niwawekee bafuni, sasa nyie wamama mnaowekewa maji ya kuoga na wasichana ndo mfunguke macho! enhee, kingine? akasema unaona hizo goroli anachezea Rayan? akasema hayo ni macho ya paka, wala sio goroli,uwiii, rafiki yangu alipiga kelele watu wakajaa,jamani sio mbali ni pale Tabata Liwiti, akasema, ukinituma kusafisha chumbani kwako nimeweka dawa chini ya godoro lenu ili" msiweze" halafu uachike,niolewe mie, uwiiiiiiii! wandugu, sio habari ya kubuni nimeona live kwa shosti wangu, kwa hiyo tunaposema spiritual screening huwa huwa ni MUHIMU SANA.
Ni pale tu uhusiano wetu na Mungu unapokuwa mzuri, ndipo tunapokuwa na AUTHORITY ya kuweza "kufanya hizo screening", maana tulipewa hayo Mamlaka in accordance with the Holy Scripture.
Wandugu,tunamuhitaji Mungu sana in every aspect of our lives, so we should be connected with Him always, huyo ni Mungu yule, aliyemzuia Balaam njiani asiende kuwalaani Israel, ni huyo huyo aliyemwonya Yusufu katika njozi,kwamba aondoke akimbilie Misri yeye na mkewe Mariam maana kesho yake Herode alipanga kuua watoto wa kiume, na huyo Mungu aweza kukuamsha wewe usiku na kukuonyesha adui anayetaka kuja kuangamiza nyumba yako, stay connected with Him always, for your safety and security.Sasa ya kumalizia, ni juzi, last saturday, nilienda kumpeleka msichana wangu kwenye maombi kanisani, maana huwa anaweweseka sana usiku. Tukafika pale, tukakuta kuna "Osigelo' anaombewa, nikamuuliza yule mama niliyekaa naye jirani, aisee huyu binti ni mwanao? akasema ni msichana wangu wa kazi, ana shida gani? akasema ni "mchawi" , umejuaje? kasema nimekaa naye wiki moja tu vitu anavyovifanya vimenipelekea kumwuliza na amekiri, vituko gani? anachelewa kurudi nyumbani asubuhi, mhh! kurudi kutoka wapi? akasema tukilala usiku huwa anatoroka, anaenda wapi? kuzimu na bibi yake? hee? Huyo bibi yake unaishi naye? hapana, huwa anamfuata usiku wanaondoka, milango yote tunafunga, lakini binti anatoweka anarudi asububi saa nne, hee? macho yalinitoka kama fundi saa! umemtoa wapi? nilimpa mtu nauli akaniletea, huko Iringa, hee? she is just 16 years old, wandugu niliona mwenyewe juzi, yule binti alieleza mambo mengi sna wakti akiombewa, na kwamba yeye mission yake ni nini anapopata kazi za ndani kwenye nyumba za watu!

Mhh! hebu leo niishie hapa, kesho tumalizie na yule wa shosti yangu wa pale Tabata mawenzi, yeye hakuwa mchawi, lakini alichokifanya, kinatisha! MY darling friends, Tunamuhitaji sna Mungu, na sio kwa wafanya kazi wa ndani tu , but hata na ndugu tunao ishi nao au wageni wanaotutembelea makwetu, hivi mnajuwa huwa wanawafanyia nini watoto wetu usiku wanapolala vyumbani kwao?


Kesho tutamalizia!

Mwenye macho haambiwi tazama!

Stella

0 comments:

Post a Comment