Friday, April 26, 2013

SHUKRANI....

Hahahahaha jamani acha nicheke maana nimefurahi jana wanawake wenzangu wamenifurahisha na kunichekesha sana mwanzoni watu mlikuwa mnasikiliza tu ila hahahaha hapana mkaamua kufunguka na kuwasha ukumbi moto kweli hapana chezea wanawake wangu..

Anyways nataka nichukuwe muda huu kuwashukuru wanawake wengi sana siwezi kuwataja kwa majina maana mlikuwa zaidi ya mia mbili kwanza kabisa kwa kuitika wito wangu kama ninavyowaita kila mwaka mara mbili mkaja kujifunza mambo ya chumbani lakini sio tu kujifunza nyie naamini ni kwasababu mnataka kwenda kuwapa wapenzi/wame zenu raha..haloooooo mwanamke maujuzi bwana akiamua kutoka na atoke lakini hakuna kama wewe..

Napenda niwashukuru wanawake waliowasha moto kuwapa challenge wake za watu ambao walikuwa wanadhani kwakupata ndoa ndio wamepata kila kitu na kuanza kujibweteka lakini kwanzia jana usiku naamini hakuna tena mwanamke atakayejibweteka kwenye ndoa yake.

Makungwi wamewafurahisha wengi mmeniambia nani kakonga moyo wako zaidi ya mwengine hao hizo ni kazi zao mimi nakazia tu kama mlivyoniona a.k.a kungwi mtoto nakaribia kupata shahada wa kuwa kungwi kamili wa mambo ya chumbani..hahahaha ngoja nijisifie babu weee inahusu

Napenda kuwashukuru kibao kata ambao walipiga sana na wanawake wote walioamka kucheza kibao kata tumeona nyonga za kila aina na mkafundishwa kukata viuno natumaini mtayafanyia kazi.

Kutokana na maombi ya wanawake walio kwenye ndoa zao nimeamua kufanya mafundo ya wanawake 100 tu walio kwenye ndoa tena haswa wanawake waliokomaa wenye uchungu wa ndoa zao na ambao wanataka kujifunza kwahiyo utakapolipia muda huo ukifika nitajuwa kama wewe umekomaa na kama unastahili ticket ya kuingia kwenye mafundo hayo kumbukeni ni watu 100 tu nikimaliza mia sitaongeza tena..nitawapa tarehe lakini ni mwezi wa SABA nitaifanya siku ya jumamosi na ni asubuhi saa tatu mpaka jioni saa kumi na mbili ili turuhusu kuendelea shughuli za familia zetu nitawapa tarehe siku zinavyozidi kuja.

Lakini mashoga zangu wengine ambao hamna ndoa sio kwamba nimewatupa tarehe yetu ya kufunda kwa ujumla tena kama ijumaa ni 13/10/2013 shughuli za mjini ni nyingi lakini naamini kama wewe unataka kujifunza zaidi ya uliyojifunza ijumaa naamini hutakosa sasa hivi tutachukuwa ukumbi mkubwa na kuruhusu watu wengi zaidi kuhudhuria, jana mlisema mnataka sare katika kila shughuli na ninakubaliana na matakwa yenu, nitaendelea kuwakumbusha zaidi ila kumbuka tu hiyo tarehe.

Namalizia jamani ndio nakubali tunaenjoy sana tukiwa pamoja kwenye mafundo, ndio nakubali kila mwanamke anayekuja na bidhaa zake pale anapata hela lakini jamani umuhimu na madhumuni makubwa ya mimi kuanzisha haya mafundo ni ili tujifunze na sio biashara na naamini wanawake wengi sana mtanipigia simu 0717 019320 na kunipa feedback ya masomo mliyopata yanavyowasaidia na hiyo ndio furaha yangu kuu.

Tukutane tena mwezi wa saba wewe mwanamke mwenye ndoa yako.

Ahsante

Reactions:

7 comments:

 1. Mafunzo ni mazuri tena sana but nilikuwa na ushauri kungekuwa na mada kuhusu biashara,malezi,usafi wetu wa majumba yetu kama kukumbushana na mwishowe mambo yetu yakikubwa zaidi...na chakula tuimprove kdg bt for start keep ut up nimependa coz ni kiswahili zaidi uzungu unahuuuuuu

  ReplyDelete
 2. Sasa ngoja niwape yaliyonikuta kuhusu kile chakula sinikajishaua kwamba ngoja ninunue kuku wa kienyeji bonge la mapande tuchome watu wajisosomole nikamlipa na mtu hela kabisa ya kunichomea kumbe na yeye asiseme hawa kuku lazima uwachemshe kwanza kidogo ndio uwachome akawachoma vilevile ndio maana wakawa wagumu vile jamani naombeni mnisamehe sana next time nitabaki tu na kuku wangu wakizungu..hiyo ilikuwa mara ya kwanza na ya mwisho kuchoma kuku wa kienyeji..

  Ahsanteni

  ReplyDelete
 3. Nimekupenda bure umetoa reason hope next tyme itakuwa funika bovu uzungu unahusuuuuuu. Na kingine maji ya kunywa ingekuwa mtu akiingia anapata moja na kwenye menu akienda pakua anakuta pia......loh mwanamke na chumbani babuuuuuu mwezi wa kumi naona mbali

  ReplyDelete
 4. Halafu chakula kilikuwa cha baridi next time jitahidi kiwe moto. Km alivyosema mdau tufundishane na mambo mengine pia. Otherwise shughuli ilikuwa pambe sana tunangoja mazuri zaidi mwezi wa kumi

  ReplyDelete
 5. TUPE FULL DETAILS ZA HIYO YA JULY TWATAKA TUJE WAPI LINI SH NGAP.....

  ReplyDelete
 6. arusha nako msitusahau jamani..umekoja mara moja..lini tena waja?

  ReplyDelete
 7. kwa sie tulio Arusha tunakusubiri kwa hamu Penguin tupe ratiba mama wa chumbani

  ReplyDelete