Monday, April 29, 2013

Mwanzo 9:20 Nuhu akaanza kuwa mkulima akapanda mizabibu, 21 akanywa divai akalewa akawa uchi katika hema yake, 22 Hamu baba wa kanaani akauona uchi wa baba yake akawaeleza ndugu zake wawili waliokuwa nje, 23 Shemu na Yafethi wakatwaa vazi wakalitanda mabegani mwao wote wawili wakaenda kinyumenyume wakaufunika uchi wa baba yao na nyuso zao zilielekea nyuma wala hawakuuona uchi wa baba yao, 24 Nuhu akalevuka katika ulevi wake akajua mwana wake alivyomtenda, 25 akasema na alaaniwe kaanani atakuwa mtumwa kabisa wa ndugu zake.

Jamani mmeona jinsi kijana alivyolaaniwa alipouona tu uchi wa baba yake katika biblia lakini maisha ya siku hizi inakuwaje, inahusu nini wewe mwanamke kulala na baba yako ama mwanaume kulala na mama yako hiyo ni laana mbele ya MUNGU na usije ukaona mambo yako katika maisha hayakuendei sana ukaanza kulalamika umelogwa akuloge nani na umejiloga mwenyewe.

Tena utamkuta mtoto haogopi jamani anajipitisha kwa baba yake kinguo kifupi huna haya, ama utakuta mtoto miaka 18 na kuendelea unamkumbatia baba yako zaidi ya sekunde moja inahusu unadhani yule sio binadamu kwasababu bwana matatizo mengine huwa tunajiletea sie mwenyewe yule pia ni mwanaume tena lijali na mashetani ya kimpanda anasahau hata kama wewe mwanaye.

Yani mimi nafikiria sana hili jambo linanikera unaanzaje kufanya vitu kama hivyo inamaana wanawake au wanaume wote wameisha jamani???

Mmmhh haya bwana kumbukeni duniani tunapita mahesabu kwa MUNGU.

0 comments:

Post a Comment