Sunday, March 10, 2013

Lako hilo kama linakuhusu....

Shalom wana wa Mungu
Kuna jambo ninapenda kuwakumbusha wadada wazuri wa Yesu. Ni sawa unaweza kuwa na namba ya simu ya mkaka labda unafanya naye kazi, mwalimu wako, mteja unapofanyia kazi, rafiki wa kaka yako n.k. Unafahamu kuwa mtu huyo ameoa na anafamilia. Sasa pale anapokutumia msg au mnachat facebook anapokuambia anakupenda na anataka kuwa nawe, tatizo linaanzia hapa.

Unakuta binti ameokoka badala ya kumkemea na kukata mawasiliano kabisa na mtu huyu kubakiza ya kikazi tu, anaendelea kumu entertain, anaendelea kuchat nae kila siku, hadi usiku. Unakuwa sehemu ya usaliti wa mtu huyo kwa mke wake, wakati mwingine anakutumia vocha, na unajua anakutaka na bado unakubali huku ukijifariji kuwa nimemwambia hapana.
Jiulize, Je unapofanya hivyo unapata ujasiri wa kusimama mbele za Mungu? Anapoongea na wewe masaa mengi usiku huoni kama unakuwa sababu ya huzuni kwa mke wake? Unajifariji unamshuhudia maneno ya Mungu, Je hiyo ndio njia sahihi ya kumhubiria mtu wa aina hiyo?Tambua wewe ni mtoto wa Yesu, usiishi kwa kuifuatisha namna ya dunia hii.
Mnisamehe leo nimekuwa mkali kidogo, ila najua kuna mtu atapata uponyaji kwa ujumbe huu.
 
Source: Women of Christ

Reactions:

0 comments:

Post a Comment