Wednesday, February 27, 2013

Nyanya chungu..

Leo wapendwa nataka niwafundishe kuhusu nyanya chungu, ndio enhe hizohizo naamini wengi kama sio wote mnazijuwa zipo za iana mbili zile chungu kabisa na za baridi (ambazo sio chungu) najuwa wengi sana hawapendi kula hizi nyanya chungu kwasababu hawazijui faida zake leo nitakwambia nisikilize kwa makini mwanamke na wewe mwanaume ukalibebe umpelekee mkeo anufaike nalo.

Nyanya chungu katika mwili wa mwanamke zinasaidia katika kuongeza maji ya ukeni enhe ndio utakuta mwanamke analalamika mimi mkavu mume wangu anachukuwa muda sana kuniandaa mwengine anasema nachubuka sina majimaji ya ukeni sasa shoga dawa ndio hiyo usikose nyanya chungu nyumbani kwako kama huziwezi chungu waachie wahaya wewe nunua zile za baridi hata kama huzipendi shoga ndio uzile mpaka uzipende, sio mbaya ukiungia kama mbili kwa kuanzia baadaye utaweza kula zidi..mimi nyumbani kwangu mwiko nyanya chungu kukosekana kwenye jokofu..haihusu bibi

Unaweza kuziungia kwenye vitu tofauti na zikanoga ngoja nikwambie jinsi mimi ninavyozitumia natia kwenye mlenda, kwenye dagaa, kwenye mboga ya nyama, kuku, natia mpaka kwenye pilau yani kila ninachopika nyumbani kwangu lazima ziwemo wanawake wote nyumbani kwangu nimewazoesha kuzila ila wanaume hawali kwanza kwasababu hawazipendi na pili kwavile haziwahusu labda kurekebisha afya tu siwalazimishi.

Umenisoma chukuwa hilo kama ulikuwa haujui..

Reactions:

0 comments:

Post a Comment