Sunday, January 20, 2013

Utafanyaje kama Ingekutokea wewe...

Dada Rose mimi ni msichana ninakaa na baba mtoto wangu hatujaoana lakini tunamtoto wa miezi mitatu sasa, baba mtoto wangu ni kijana ambaye anajipenda sana yani yupo very smart sijawahi kuona kijana anayependa kuvaa nyeupe na siku zote akarudi mtanashati kama baba mtoto wangu.

Kipindi alivyoanza kunitongoza na kukubaliana kuwa wote nikawa nasikita tetesi watu wakisema kwamba baba mtoto wangu sio riziki, sikutaka kusikiliza maneno ya watu kwani kama kunipenda alikuwa anipenda sana na kama kunitimizia kitandani alikuwa ananitimizia sana.

Muda ukaenda nikagundua nina mimba ndipo tulipoamua kuhamia tuishi pamoja maisha yaliendelea vizuri tu na mapenzi yakawa motomoto mpaka nikajifungua mtoto wa kike ambaye kwa sasa anamiezi mitatu ila kunamabadiliko ambayo nimegundua kwa mwenzangu, anapigiwa simu usiku na wanaume mara anavaa na kuondoka na kuniaga anaenda kwenye madili ya kutafuta pesa basi nami kwa vile nilikuwa nyumbani kazini siendi nikawa nakubaliana nayo. 

Kumbe kweli baba mtoto wangu analiwa na wanaume wenzake siku dada nimekaa nyumbani yeye hayupo mara wakaja wageni wanaume wawili na kuniambia wanamtafuta baba mtoto wangu nikawaambia hayupo kwa jazba na hasira walizokuwa nazo hawakuweza kuvumilia na kuniambia kwamba wanamdai hela kila mtu 50,000/- ambayo aliwaahidi kuwapa kama watamshughulikia!!!!! dada nilivyosikia hiyo habari nilitaka kufa tumbo liliniuma kama lauchungu na wakaniambia wanapajuwa hapo nyumbani kwake kwasababu kabla ya mimi kuhamia walikuwa wanakuja kumshughulikia hapo.

Kwakweli baada ya hao wakaka kuondoka nilipatwa na msongo wa mawazo nilihisi kufa nikaanza kufikiria yale maneno niliyokuwa naambiwa mwanzo na watu kuhusu mpenzi wangu, Aliporudi nyumbani nikaongea naye kuhusu hilo swala kwa mara ya kwanza hakunificha akaniambia ni ukweli.

Nilitaka kufa maana nikaona hii ni aibu gani nimejiingizia familia yangu watanionaje kwamba nimezaa na mwanaume anaye kula na kuliwa kwakweli hiki kitu kilinichanganya sana na  nikaamua kwenda kuongea na mama yake kuhusu hilo swala ndipo mama yake aliponifungulia ukweli kuhusu mwanaye na kwamba alishamuonya lakini hakusikia sasa wanataka kumkalia kikao wanafamilia wamtoe katika ukoo.

Dada mimi nimeshazaa na huyu kaka familia yangu wanajuwa nakaa naye na alikuwa na mpango wa kunioa nampenda sana lakini siwezi kukaa nikijuwa analiwa kila nikifikiria starehe ninazozipata katika mapenzi na nikifikiria na yeye anaenda kupindwa na kupewa na wanaume wenzake kinanichanganya sana namuonea sana huruma mwanangu kulelewa bila baba ila nimejipanga nataka kuondoka siwezi kuishi naye huku tena huo ndio uamuzi wangu.

Nilimuona mtanashati anapendeza na kuvutia nikajuwa nimepata, kumbe ananila na yeye kwenda kuliwa ee mungu wangu nisaidie niweze kupita vyema hiki kipindi kigumu sina la kuwaambia wazazi na rafiki zangu kwanini hawatamuona tena kwa sasa bado nafikiria ugomvi wa kuuanzisha ili wasipate pa kunirusiha naye kuomba msamaha sitaki wajuwe tatizo lake kwani hata kama nimekasirika na kuondoka sioni sababu ya kumdharilisha.


Reactions:

0 comments:

Post a Comment