Thursday, January 31, 2013

Msaada Tutani....

 swali naombeni ushauri haswa kwa madaktari kama wamo humu eti ni kwanini mnakataza mama mjamzito kukandwa maji akiwa ametoka kujifungua wakati mama huyohuyo akirudi nyumbani hukandwa maji ya moto sana ili kuondoa damu za uzazi na kurudisha mwili sawa na pia hushauriwa kunawia hayohayo maji ya moto ukeni ili paweze kurudi kama mwanzo.

Na pili nasikia mtoto wa kiume hatakiwi kuogeshwa maji ya moto nasikia anapoanza kukomaa unatakiwa kumuogesha na maji ya baridi kwa kuwa ya moto yanamvunja nguvu za kiume kuna ukweli wowote katika haya????


4 comments:

  1. Mimi sio dr ila mama yangu dr ninavyofaha ukifanyiwa operesheni ndio hukandwi wengine wote tunakandwa coz nina mtoto na nilianza kukandiwa hosp kuhusu mtoto wa kiume ni imani tu za watu mtoto ataogeaje maji ya baridi nimonia itamuacha kweli

    ReplyDelete
  2. Mtoto wa kiume hafai kuogea maji ya moto kwasababu ili korodani ziproduce mbegu zenue uwezo na afya inahitaji optimum temperature.Ila anaweza ogea maji ya uvuguvugu kama kiwango cha body temperature ya binadamu

    ReplyDelete
  3. Maji ya moto yanasaidia kutoa damu ya uchafu unapokandwa na sina hakika kama yana madhara,kuhusu mtoto wa kiume kama alivyosema madau hapo juu ni imani tu.

    ReplyDelete
  4. Mimi binafsi nimejifungulia nje ya nchi na sikuwa na msaada wa ndugu au jamaa wa karibu wa kunifunza mambo ya kimila. Huku hakuna kukandwa wala si lazima kutumia maji moto. Hospitali wanakusaidia uoge na maji vuguvugu baada ya kujifungua, alafu baada ya hapo unatakiwa uoge na kujinawisha vizuri sana kila siku ili usipate infection.

    ReplyDelete