Thursday, January 31, 2013

Uganda ugomvi wa wanandoa wafichua makubwa.....

Emmanuel Kalema akiwa akimezungukwa na wananchi wenye hasira kali.
Wanandoa waliofarakana nchini Uganda wamewashangaza wakazi wa manispaa ya Nakawa, Kisenyi Zone.
Kulitokea kutoelewana baina ya Emmanuel Kalema (32), na mkewe aliyefahamika kwa jina moja la Aisha (28) hivyo mama huyo kuamua kufungasha vitu vyake na kutaka kuondoka na watoto wao ndipo ghafla Kalema aliporopoka kuwa akitaka kuondoka na watoto basi amchukuwe na Yule waliyemuua na kumzika katika msingi wa nyumba yao iliyopo Kireka-Banda. 
Maneno hayo yaliushangaza umati uliokuwa ukishuhudia ugomvi  huo hali iliyopelekea watu kumzonga jamaa huyo na kumtaka atoe maelezo vizuri kuhusiana na mauji hayo.
Akiwa chini ya shinikizo la wananchi alisimulia kuwa yeye na mkewe walishirikiana kumuua mtoto wa nje wa mama huyo na kumzika kwenye nyumba hiyo ili waanze maisha mapya ya ndoa.
Baada ya kupata taarifa hiyoi wananchi walichukua majembe na kuanza kuchimba eneo lilitajwa na hatimaye walikuta mfuko wa plastiki ukiwa na mabaki ya mtoto huyo.
Kalema yuko chini ya ulinzi wa polisi na uchunguzi juu ya tukio hilo unaendelea.

0 comments:

Post a Comment