Tuesday, December 11, 2012

Msaada Tutani....

Habari,

mimi ni mwanamama nina mtoto mmoja. nimeolewa ndoa ya serikali kwani mimi nilikua muislam na mume wangu mkristo. tunaishi Morogoro na ndoa ina miaka 7 sasa. tulipata ushauri wakufunga ndoa ya katoliki ili mume wangu aweze kujumuika na masuala ya kikatoliki na mimi nibatizwe nimekubali.

kabla hatujafunga ndoa hiyo ya kanisani, tumekua na kutoelewana kwa muda sasa..Mume wangu si muajiriwa anafanya biashara ambazo ni za wazazi wake kwa maana yeye ni msimamizi na anapata kiasi kidogo cha pesa kwa ajili ya sisi yaani mkewe na mtoto. mimi nimeajiriwa ila sina kipato kikubwa. kwakweli wazazi wake wameshikilia maamuzi ya mume wangu na inafikia hatua mipango tunayopanga haiendi shauri ya hilo.

mimi ndo nalisha familia, na majukumu mengi sana. sasa mtoto ameanza shule hata ada hatoi. pesa yote inaenda kwao na yeye ana madeni kila siku. nilimshauri aache hiyo biashara waajiri mtu wa kusimamia ili yeye atafute mtaji au kazi yoyote ili awe na maamuzi ya pesa yake tujijenge kama familia pia haafiki hilo suala kwamba yeye lazima afanya hiyo kazi.

maisha hayana raha, sasa mimi ninapata wasiwasi je, nikifunga ndoa hiyo itakuaje na naona kama muelekeo haupo wa yeye kutujali sisi. na huwa natamani hata niachane nae nilee mwenyewe mtoto maana ni mzigo kwani ndugu zake nawalisha mimi pamoja na huduma nyengine.


naomba unishauri kabla sijatumbukia humo. tafadhali nishauri na unaweza kuipost wengine washauri pia.



Clare!

6 comments:

  1. pole mamii,chakufanya hapo achana na huyo mwanaume lea mwanao wanawake tuko juu tunaweza bila wanaume janaume zigo alafu jeuri pia achana nalo kma bishi lea mwanao na fanya kazi kwa bidii si kila anayevaa suruali ni mwanaume wengine siyo mamii.pole weeeeeeee. achana nae kabisa yaaaaaaaaaaani.mwanaume mwenye akilia zake kwanza hawezi kufanya buzness za nyumbani kwao hawazi mbele huyo anawaza karibu so hilo ni zgo la mavi.amka mama.from mama sasha

    ReplyDelete
  2. Pole mamii..

    Mpenzi ndoa inamambo mengi sana yaani mara nyengine ukifikiria unaweza kutaka kuondoka na kuiacha.

    Najuwa upo kwenye maumivu na unahisi kama mumeo hakupendi kabisa ndio maana hasikii unalomwambia lakini nataka nikwambie jambo moja ya kwamba mumeo sio kwamba hataki kutafuta kazi nyengine ili awatunze nyie anaile hofu moyoni kwamba itakuwaje akiacha kufanya kazi kwa wazazi wake na akiangalia biashara hiyo ndio iliyomkuza mpaka akaoa ni ngumu sana.
    Lakini lazima ukomae naye kwamba kama anaona hawezi kuachana na wazazi wake basi atafute biashara pembeni ya kufanya ili muweze kuendesha vyema familia kwasababu hata siku moja mkono mmoja hautoshi kuendesha familia.
    Lakini pia kumbuka mna mtoto usifanye maamuzi ya kujiangalia wewe kwanza angalieni huyu mtoto anayehitaji malezi ya baba na mama kama wewe unakazi na badi haikutoshelezi jaribu kufanya na biashara nyengine pembeni siku hizi unaweza ukawa umeajiriwa na pia ukafanya na biashara ya pembeni mimi mwenyewe nimeajiriwa na pembeni nina biashara zangu tatu ili nisaidie nyumbani kwangu.
    Ni kweli wanaume wakati mwengine hawana kabisa hata akiwa hajaajiriwa na wazazi, kipindi kingine madili hamna kabisa utasubiri atafute kazi halafu mfe njaa hapana utasimama kama ubavu wake pale unapoweza utasaidia maisha yaende mbele kama yeye hatadhamini mchango wako leo lakini MUNGU aliyewaunganisha atakuzidishia na kukupa baraka tele kwa kuilinda na kuitunza familia yako kama msaidizi wa mumeo

    ReplyDelete
    Replies
    1. My dear Rose sorry nilikua mbali na kupata mtandao. Asante sana kwa ushauri. Yani nitaufanyia kazi. Maisha ni changamoto. Nitapambana tu

      Delete
  3. Pole my dia kwa maelezo ulotoa la kazi ni moja linalokuumiza lakini inaonekana kuna mengi hamsikilizani, wewe ndo wajua. Mtoto anahitaji malezi ya baba na mama, malezi ni nini? ni uwepo tu?ni maneno au ni vitendo mimi sijui ila mwaelekea kwenye ndoa kama kuna tatizo fix it now or let it for good. Ongea nae ukimwangalia usoni kwa staha ofcourse, mwambie abadilike na mjipange kama familia vinginevyo ni ngumu. zaidi sana mtangulize MUNGU.

    ReplyDelete
  4. pole sana Clare.

    maisha ya ndoa yanataka uvumilivu na kumwomba Mungu sana,kwenye uvumilivu namaanisha usichoke kumshauri mumeo kila kunapokucha,mfano mimi mume wangu alivyonioa alikuwa amejiajirini so kipato kwa familia kilikuwa kidogo sana,nikimwambia mambo ya ajira hataki kabisa,nilisali sn maana mimi nafanya kazi.wakati mwingine mimi ndio inabidi niwe nalisha familia maana mwenzangu hajapata kazi kwenye hiyo kampuni yake.kuna vikundi vya maombi sikuchoka kuwashirikisha kuomba nami,na kila siku nikimpa faida za kuajiriwa serikalini.kwamba anaweza kuajiriwa na akaendelea na kampuni yake kama kawaida,yaani hadi akaingia line,now ameajiriwa na anaendeleza kampuni yake.mpaka siku moja akakiri mwenyewe kwamba MWANAMKE NI NGUZO KWENYE FAMILIA na wanaona mbele.sasa tunamshukuru Mungu familia inafuraha tele.tumejaliwa mtoto mmoja na tumeanza ujenzi wa nyumba.
    usichoke kumshauri mumeo maana sisi wamama ndio washauri wakuu wa waume zetu,pia uwe mvumilivu my dear huku ukimuomba mungu kila siku.

    ReplyDelete
  5. Haina haja ya kutoka kny dini yako hapa na kujipa kitanzi cha TILL DEATH.. huko katoliki mwelekeo kashakuonyesha sio mzuri sasa umfate wa nn fanya yako lea mwanao panga mipango yako mikubwa ya maendeleo usimshirikishe mwangalie2 na hao ndugu zake komesha hamna kuwapa msaada

    ReplyDelete