Tuesday, December 11, 2012

Tahadhari Wazazi......

Hivi karibuni vyombo tofauti vya habari vimeripoti kugundulika kwa mtandao wa kuiba watoto baada ya kubainika kuwepo kwa nyumba inayotumika kuhifadhi watoto wanaoibiwa jijini Dar es Salaam.

Watu hawa wanawafuata watoto shuleni hasa saa ya kutoka na kufanya wanawajua, na wengine kufanya wanawasaidia kuwavusha barabara na baada ya hapo kuwaahidi kuwapa hela na vitu vingine.Wanawachukua watoto na kuwapeleka kwenye nyumba hiyo na kuwafungia humo.

Hadi sasa haijafahamika wanawafanya nini baada ya hapo, na wala watu hao hawajakamatwa bado.Hivyo wazazi tuwe makini katika uangalizi wa watoto wetu hasa ukiona muda wa kawaida wa mwanao kurudi nyumbani na bado hajarudi.

Pia tuwafundishe watoto kutokukubali kuchukuliwa na mtu yeyeto ambaye hajawahi kumwona hata kama atamwita kwa jina lake.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment