Wednesday, December 26, 2012

Kuna siku moja mimi na wanangu tulienda kumtembelea rafiki yangu mmoja nyumbani kwake, tukashinda huko siku nzima rafiki yangu huyu ameolewa na anawatoto wawili wakike na wakiume.

Kabla hatujaondoka kunakosa mtoto wake mmoja alifanya na mama mtu akawa anamkanya lakini hakusikia kutokana na hayo akachukuwa mwiko na kumchapa yule mtoto na baada ya kuchapwa kweli yule mtoto aliacha lile jambo alilokuwa anakatazwa kufanya na mama yake na chakushangaza watoto wangu walivyoona mwenzo anachapwa na mwiko wakaogopa sana na mimi moyoni nikafurahi ya kwamba nimepata kitu cha kuwatishia wanangu wakiwa hawasikii maana jamani watoto wangu ni watundu na kiburi ndio usiseme sijui wamerithi wapi.

Basi kuna siku mwanangu wa kike na yeye akaniletea kiburi nikamwambia msichana wangu wa kazi aniletee mwiko basi kusikia vile akaanza kuomba msamaha akilia hatarudia tena nikafurahi kweli kwamba nimepata kiboko yao huo mwiko sasa, cha kushangaza mtoto wangu wa kiume hata ukimtishia vipi hana habari na huo mwiko wako mpaka nikaanza kumchapa nao sasa akawa analia halafu mara nyengine anarudia tena kosa na mimi nikawa akirudia siku nyengine nachukuwa mwiko tena namchapa mpaka anaacha.

Siku moja nilikuwa nazozana na wanangu nje, sisi kwetu bwana ni uswahilini sana chezea mabibo na nyumba yetu ni ya wazi tu hamna geti kwahiyo kila unalofanya barazani kwenu mtu akipita anaona, anyways basi majuzi mwanangu wakiume kuna kosa aifanya na siku hiyo nilikuwa nimekaa nje na mke mwenzangu (mke wa shemeji yangu) nikamwambia dada lete mwiko nimchape pasua maana kwajinsi alivyokuwa mtundu mpaka tumemtunga jina la pasua.

Dada akanipa mwiko nikamchapa pasa kidogo akapita mama mmoja hivi akaniona nilivyokuwa namchapa mtoto wangu wa kiume na mwiko akanifwata na kuniambia mama khloe acha kabisa kumchapa mtoto wa kiume na mwiko!!!!!nikamuuliza kwanini akaniambia mtoto wakiume unapomchapa na mwiko unamvunja ngu za kiume!!!!!!!!eenehhee ndio jamani nilishangaa kitu ambacho wewe unaona ni adhabu kumbe kinaweza kikawa na madhara makubwa nikamuuliza na mtoto wa kike akaniambia haina madhara kwa mtoto wa kike nikamuuliza kwahiyo mtoto wa kike nguvu zikimuisha sio mbaya hakunijibu alichoniambia nisimchape mtoto wa kiume na mwiko..Makubwa

Haya mama kama na wewe ulikuwa na tabia kama yangu ya kumchapa mtoto wa kiume na mwiko japo kidogo atambue kosa naomba uache tena uache kabisa ni vibaya.Reactions:

4 comments:

 1. Aisee dada asante. Na mimi ndo mtindo wangu mana mwiko c hauvunjiki upesi. Loh nimekoma

  ReplyDelete
 2. Lakini kuna ushahidi wa kiafya na wanaosema hivyo wana uchunguzi wa kutosha nafikiri ni lazima kupata maoni ya watalaamu na kutoa habari kuhusu haya mambo

  ReplyDelete
  Replies
  1. Bugando health movement perspective yako ni interesting sana. Naomba utueleze kitaalamu zaidi athari zinazotokana na kumpiga mtoto na mwiko. Pia ukiweza naomba pia ueleze namna laana ya kitovu inatokea biologically kwa mwanaume. Nitashukuru sana kujifunza kupitia maoni yako maana ninatambua kwamba baadhi ya mila zetu zina ukweli wa kibaiologia.

   Delete