Wednesday, December 26, 2012

Msaada Tutani...

Shikamoo dada Rosemary,

Kwanza kabisa ningependa kukupongeza sana kwa nafasi ya kutuelimisha wanawake kupitia Mwanamke na Nyumba. Kwa kweli kama binti ambaye bado hajaolewa nimejifunza mengi mazuri ya kuniandaa kuwa mke na mama mwema.

Kwa kweli mimi swali langu ni dogo ila naomba nikuulize maana sijasikia ikizungumzwa mahali popote na ninahope wewe kama kungwi utakuwa na a unique perspective. Nina rafiki yangu ambaye tokea sekondari ya boarding alikuwa anapenda kusugua chuchu zake ili asikie raha ya kimapenzi. Hadi hapa alipo yupo chuo na ni bikira anayekaribia kuolewa ila anaogopa kama tabia yake ya kusugua chuchu zake itamuletea madhara kwenye ndoa. Naomba dada Rose unisaidie kumsaidia rafiki yangu ili tujue:

1. Je tabia yake ni ya kawaida kwa wanawake ambayo ni bikira wanapopata hamu ya kimapenzi?

2. Kama tabia yake ina madhara mbeleni kwenye ndoa afanyaje ili aache?

Nitashukuru sana kwa jibu lako dada Rosemary na ukipenda unaweza ukaliweka kwenye blog yako kwa njia yoyote unayoona itasaidia kuelimisha umati.

Ubarikiwe sana mama na heri ya Krismasi na mwaka mpya.

Wako,

Elizabeth

Reactions:

2 comments:

 1. Elizabeth ashante sana kwa salam zako na kuwa mmoja wa mwananyumba mwenzetu katika kuelimishana..

  Sasa mamii kuhusu rafiki yako hiyo tabia yake ya kusugua chuchu sio ya kushangaza ama ni mbaya hapana mwanamke yeyote anayefikia kipindi cha kutamani mapenzi au anapofikia wakati anajitambua kwamba anamabadiliko katika mwili wake wa kumtamani mwanaume huwa anatokea kuwa na tabia fulani tofauti katika mwili wake ili kujimalizia tamaa yake japo akiwa hataki kutoa bikra yake, hilo ni jambo la kawaida na ni wanawake wengi wamelipitia sema kila mwanamke anapitia kwa aina yake tofauti.

  Kuna rafiki yangu namjuwa yeye alikuwa akisikia hamu anabana sana miguu mpaka anafika kileleni, mwengine namjuwa yeye akisikia hamu ya mapenzi anajisugua ukeni mpaka anafika kileleni lakini hao wote walikuwa bikra kipindi hicho kwahiyo nataka ujuwe hilo ni jambo la kawaida katika maisha ya mwanamke anapokuwa.

  Kama itamuadhiri katika ndoa yake sinauhakika na mume atakaye muoa atalichukuliaje hilo lakini katika mapenzi mamii lazima uwe muwazi na unachokitaka ujifanyie ama ufanyiwe katika mwili wako, kwa mfano kuna wengine mwanaume akiwa ameingia ndani yeye bado hujisugua uke ili apate raha zaidi na wengine hujisugua chuchu kama rafiki yako hiyo sio mbaya muache kama inampa raha aendelee nayo na inaweza ikawa kichocheo kikubwa cha kumfanya mumewe aendelee kupata hamu ya kuwa naye katika mzunguko kwani inamrahisishia mumewe kama mke akifanya hivyo anasikia raha.

  Cha muhimu mwanamke lazima uwe muwazi usiogope kwani mzunguko wa uwazi ndio utaenjoy kuliko kujificha ukiogopa utaonwa wa ajabu.  ReplyDelete
 2. Asante sana dada Rosemary kwa kujibu maswali ya mimi na rafiki yangu kwa ufasaha wa hali ya juu. Ninakutakia tena na tena mema katika kazi yako ya kutuandaa mabinti kuwa wake na mama wema mbeleni.

  ReplyDelete