Thursday, November 1, 2012

 “UKIONA mwezio ananyolewa na wewe tia maji maana yake kuna siku nawe yanaweza kukufika.”

Hiyo ni kauli ya mama aliyejitambulisha kwa jina la Felister Ramadhan kutoka mkoani Manyara ambaye amefika jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kumuuguza mwanaye anayeugua bandama na ini.

Felister aliliambia gazeti hili maeneo ya Tegeta Msichoke katika Manispaa ya Kinondoni hivi karibuni kuwa, mwanaye aitwaye Magdalena Daniel (7) hali ya afya yake ilianza kudhoofu alipofikisha miaka miwili tangu kuzaliwa.

Mama huyo kwa masikitiko makubwa alikuwa na haya ya kusema:“Tatizo la mwanangu ni bandama na ini. Vipimo vilionyesha viungo hivyo vina matatizo, nikashauriwa nije katika hospitali kubwa ndiyo maana nipo hapa.

“Mimi sina uwezo wa kugharamia matibabu na mume wangu naye ni mgonjwa, niliamua kuja Dar lakini ile nauli ya kwenda Hospitali ya Muhimbili nayo inanishinda.”

Naye Mjumbe wa Serikali ya Mtaa wa Tegeta Msichoke, Clemence Ngusa alimwambia mwandishi wetu kuwa ni kweli mama huyo anashindwa kupata nauli ya kumpeleka mwanaye Muhimbili kutokana na uduni wa maisha.

“Upande wa serikali ya mtaa, hatuna fungu, nawaomba wasamaria wamsaidie ili mtoto aweze kutibiwa,” alisema Ngusa.

Kwa yeyote aliyeguswa na habari ya mtoto huyu awasilinane na mama yake kwa simu namba 0688 17 02 12.

Source:Global Publishers


0 comments:

Post a Comment