Wednesday, October 31, 2012

KUFUNDWA...7/12/2012 lipia nafasi yako sasa

Wapendwa kwanza kabisa naomba mnisamehe kwa mabadiliko yaliyojitokeza lakini hayo yote ni kwasababu tu nataka tufanye kitu ambacho mtu atakapotoka aone umuhimu wa kuhudhuria siku nyengine kwamba kitu kimependeza na mmefurahia.

Shughuli yetu imebadilika tena tarehe kwenda siku ya Ijumaa tarehe 7/12/2012 na haitabadilika tena itafanyika pale The majestic hall sinza kwa remy kwanzia saa kumi na moja mpaka saa nne usiku ili tuwahi visa zetu (wale wake za watu ndio hupewa visa) na wengine wanaotaka kumalizia siku disco waweze pata muda wa kujiandaa vizuri maana wengine watakuwa wametoka kazini moja kwa moja.

Jamani siku hii ile ya tuliyofanya mwanzo cha mtoto humu mambo balaa nasema tena kama wewe unaaibu haikufuai na kama wewe unahisi hujakomaa bado mtoto baki nyumbani huku kwa watu wazima  wanaojipenda, wenye kupenda wapenzi wao, na kukataa wapenzi wengi kuepusha UKIMWI maana hapa tutafundwa jinsi ya kumpa raha mumeo ama mpenzi wako ambaye unatarajia atakuoa siku moja maana inaweza ikatokea mpaka mtu kuvua nguo kutufunda vyema ndio maana kama wewe sio mtu mzima uliyekomaa usije, unaambiwa heshima ya mwanamke uwe mke sio uchukuliwe tu poapoa kama juisi ya embe ukimaliza kunywewa nzi wanasafisha glass..

Kutokana na mawazo ya wengi wanasema bora tuwe na sare kama ni moja kama ile ya mwanzo ya madira meusi na gold tulivyopendeza basi mimi na kamati yangu tumeona tubadilishe kiingilio na kuwa 35,000 na sio 30,000 ili upate na kikoi chako ambacho ndio sare halafu juu utatupia vest nyeupe au singlendi kama wabongo tuvyoziita kwahiyo utapata sare yako.

Wanawake kujiamini kwako sio kwa kisomo na kazi tu, mwanamke heshima yako uitwe mke wa fulani na MUNGU akipenda mama fulani.

Tukutane tarehe 7/12/2012 wapenzi na MUNGU awabariki


Reactions:

1 comments:

  1. Kama bunduki haina risasi itauaje??

    ReplyDelete