Saturday, November 3, 2012

Mwanamke raha jamani..

 hehe heiya jamani nakuletea kwenu sufuria, najuwa wote mtakuwa manaijuwa sufuria kwasababu kila mmoja kwao anayo labda kama unakaa uzunguni huko maulaya na uarabuni mtakuwa nazo za kisasa zaidi kuliko hizi zetu siye tulizozizowea za kibongobongo.

Raha ya sufuria bwana ujuwe kuitumia tena kwa heshima sio unaitumia unaibwaga hapo unaondoka zako shoga huo uchafu tena aibu kwako, kwa mumeo/mchumba wako na huko ulikotoka kama hukufundwa ila kwakuwa maisha ni kujifunza kila siku ndio maana tunakuwa wote na kufunzana kila mara..

Shoga unajuwa kuiosha sururia ama ugali ukiganda ndio basi huwezi tena kuisugua unaitia maji madai yako nitaipikia tena nitaiosha vizuri kwani nani anayejuwa jiko si langu..hehe heiya shoga aibu shoga sufuria inasehemu sita kuu za kuiosha unazijuwa?? susfuria haioshwi nje tu kuna sehemu nyingi ili iwe safi na uitake kuitumia hata mumeo akipita jikoni afurahie mahanjumati utakayompikia na sufuria yako..

Unazijuwa hizo sehemu tofauti, na unazioshaje na wakati gani.......NAJUWA NIMESHAKUACHA KWENYE MATAA.....SIENDI NJIA HIYO ULIYOPO GEUZA SHOGA....

Tukutane 7/12/2012 tukupe raha ya kuwa mwanamke..

Reactions:

0 comments:

Post a Comment