Friday, November 2, 2012

Mmmmhhhh

Yani jamani sisi wa dada mara nyengine tunavituko kweli jamani yani naandika haya mpaka nasikia kulia, kuna mkaka alipata mwanamke huyu mwanamke nyuma alishazaa watoto wanne sina uhakika kama wote ni baba mmoja ama tofauti ndipo alipokutana na huyo kaka wakapendana na kaka akamkubali pamoja na watoto wake hao wanne.

Wakawa pamoja kwa kama mwaka na nusu baada ya kujipigapiga huku na kule yule kaka akaamua kwamba muda umefika wanunue kiwanja halafu wajenge, basi kwavile wote walikuwa na biashara zao yule kaka akaamua kununua kiwanja kwakuwa kilikuwa cha bei juu kidogo hakuweza kumalizia kwahiyo yule dada akaamua kuongezea hela na kukinunua.

Baada ya kukinunua wakaanza mkakati wa kujenga wakakijenga na nyumba ikaisha nyumba ilivyoisha yule mama akafanya juu chini akapata hati ya nyumba akaenda alipoenda akaibadilisha na kuandika jina lake bila kumwambia mwenzake.

 
Baada ya muda yule dada akaanza kubadilika na kumfanyia yule kaka vituko, visa na masimango ikafikia kipindi mpaka yule dada akaanza kumwambia yule kaka bora wauze nyumba wagawane hela kila mtu afe kivyake!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! yule kaka akawa anakataa basi yule dada ndio kumpasulia kwanza unakataa nini wakati nyumba inajina langu naweza kuuza na nisikupe kitu nakuonea huruma ili tugawane hela unaleta ubishi..ndio yule kaka wa watu kushtuka alichofanyiwa na yule mwanamke.

 
Yule kaka tena akawa hana raha ya kukaa pale vituko vimezidi jumatatu jioni akachukuwa uamuzi mgumu na kuamua kujinyonga!!!! jana ndio wamemzika yule mwanamke hata hakujisumbua kwenda kumzika mpenzi wake na wala haijulikani halipo.

Yani kweli jamani mtu umepata mwanaume aliyekukubali na watoto wako wanne halafu unamfanyia vituko mpaka ajiuwe...jamani kweli kunawatu wanaroho za ajabu yani kwenye msiba hakuna hata aliyelia kwasababu watu wote walikuwa kwenye mshtuko na maulizo mengi.Reactions:

0 comments:

Post a Comment