Tuesday, November 6, 2012

Vituko Uswahilini...

Unaambiwa uswazi tuachie wenyewe waswahili, kasheshe uswahilini kwetu leo jamani kabla ya kuanza kuhadithia hii story ngoja nikuulize unajiamini vipi wewe kama mke? ama mchumba unayetaka kuolewa ama hata kuoa maana kumbuka wengi sana wanataka hiyo nafasi yako lakini hawana, hawajapata wa kuwaoa ama kuolewa nao sasa wewe unajichukuliaje ama poapoa tu..asubuhi maziwa usiku tui?

Kuna dada mmoja uswahilini kwetu yeye ni mchumba tu wa mtu ila anakaa na huyo mwanaume anayetaka kumuoa, wamekaa pamoja kama miezi tisa hivi sasa, siunatujuwa siye wanawake haswa wa uswazi kwa midomo? basi na yeye shoga kama kawaida yake pia mdomo anao na unajuwa kabisa ukishakaa sehemu kuna watu ambao utapatana nao na wengine hutopatana nao jinsi ya wewe utaishi vipi nao ndio mtihani wako.

Shoga ukikaa uswahili kila mwanamke lazima ukae naye vizuri shoga uswahilini kuna mambo, wakikuona unaringa watakutafutia sababu tu yakukunyoosha, basi bwana mwanamke yule kujifanya tena mtoto wa geti kali ndani ya uswazi kuingia na kujifanya yeye ndio yeye akipita sehemu kuna watu kusalimia mpaka atake yeye, kuna ishu ya mtaa inataka wamama kufanya mpaka ajisikie yeye basi full uzungu.

Mwenzangu waswahili wakakaa kitako na kumuundia tume!!!!!!!! siku shoga anataka kutoka chumbani aende zake kuoga maana bafu la nyumba yao lipo nje akakutana na nyoka anaingia ndani ndio kuanza kupiga makelele na kuomba msaada, vijana wa mtaani kama kawaida wao dayworker wakale basi wakamsaidia shoga huku na kule kwani yule nyoka alionekana!!! mmhhhh kwasababu mimi na wake wenzangu tumezoeana naye jana akaja kutufwata na kutuambia kihoja kingine eti anawashwa sana chini kwa bibi tokea juzi halafu katika kufungua nguo zake avae akagundua nguo yake ya ndani imechanwa katikati pale kwa bibi hicho kipande hakipo na kweli kuja kutuonyesha hichi kipande hakipo!!!!!!!!!!!!!

Jamani kama MUNGU amekusaidia ukakaa uzunguni ama nyumba ya kujitegemea mtoto ndani ya geti huna tabu na waswahili shukuru sana jamani uswahilini kuna vituko, mtu usifanye yako watakupaparaaa wee wakuchokonoe ilimrani tu basi shoga sasa hivi kaanza kuhisi watu hawamtakii mema kisa ametangaziwa ndoa.

Kama kwenu pia kunavituko tumwagie kwenye email tuvunje mbavu hapa.

Reactions:

1 comments:

  1. duh hii noma!kweli uswahili vituko vya haja,pole mrembo

    ReplyDelete