Thursday, November 15, 2012

Mwamini Mungu...

Katika hitaji lolote ulilonalo, mwamini Mungu kuwa kwa wakati wake atakupatia. Usiwe mtu wa kukata tamaa na kutafuta njia za mkato. Mara nyingi huwa tunajaribiwa kwa sababu ya tamaa na uhitaji uliopitiliza. Msichana anapoona kama hataolewa anaamua tu kukaa na mtu anayenyanyasa na kutomuheshimu sababu tu amekata tamaa.
ZAB. 62:5-6

Nafsi yangu, umngoje Mungu peke yake kwa kimya.

Tumaini langu hutoka kwake.

Yeye tu ndiye mwamba wangu na wokovu wangu,

Ngome yangu, sitatikisika sana.

Mungu anakuwazia yaliyo mema, usikate tamaa ukaamua kupita njia ya mkato, Bwana hachelewi wala hawahi.

2 PET. 3:9Bwana hakawii kuitimiza ahadi yake, kama wengine wanavyokudhani kukawia, bali huvumilia kwenu, maana hapendi mtu ye yote apotee, bali wote wafikilie toba.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment