Thursday, November 22, 2012

Majangaaa..

Kuna familia moja. Mume alikuwa na wake wawili. Ameishi nao kwa muda mrefu. Mke mkubwa amezaa naye watoto wanne na wa mwisho ana umri wa mwaka mmoja na mke mdogo ana watoto wawili. Siku moja mke mkubwa alikuwa amesafiri.

Mume katika pekua pekua akakuta nyaraka zinazoonesha kuwa mkewe anatumia ARVs. Mume anasema alipanic na kuchukua nyaraka hizo akazipeleka kwa rafiki yake ambaye ni daktari, akathibitishiwa kuwa mkewe atakuwa amejiunga na mpango wa kutumia dawa hizo za kuongeza maisha.

Yule mwanaume anasema kilichomshangaza ni kuona mkewe akitumia dawa peke yake bila kumshirikisha. Anasema aliingiwa na mawazo ya kunywa sumu. Huyo daktari ambaye ni ndugu yake ilibidi amshauri aende kuwaona washauri wa Angaza. Wakati huo mkewe alikuwa hajarudi. Yule mwanaume alikwenda na akashauriwa apime ili kama ameathirika pia, ajiunge na mpango huo wa ARVs mapema.

Baada ya vipimo, majibu yalikuwa NEGATIVE akaambiwa akae miezi mitatu arudi; alipopimwa tena akakutwa majibu hayo hayo hana virusi. Ndipo ikabidi amweleze mkewe wa pili wakaenda wote Angaza, naye akapima akakuta pia hana Virusi. Watoto wote wadogo wamepimwa pia wamekutwa hawana maambukizi.

WEWE MWANANDOA HIKI KISA UNAKIONAJE? KINAKUPA CHANGAMOTO GANI? KAMA NI WEWE MWANAUME, UNGEMFANYEJE HUYO BI MKUBWA?

Reactions:

0 comments:

Post a Comment