Wednesday, August 8, 2012

Msaada Tutani....


Dada Rose,

mie nimeolewa nina watoto 2 lkn sina amani na ndoa yangu ndugu wa mwanamme wamenishinda yaani wamenikaba koho sina amani sina raha ya ndoa yani npo npo tu yaan hata hamu ya kuchuma tunda na mume wangu haipo tena Mimi ndoa yangu inamiaka 7 na tokea nimeingia kwenye ndoa sikuwahi kuishi mm na mume wangu tu,siku zote nyumba imefulika ndugu wa mume na sio kwamba siwapendi la hasha!mambo wanayonifanyia ndio yanayosabisha nikoseamani na ndoa yangu yaani 
vijimanenomaneno vya kila siku visivyokuwa na kichwa wala miguu na ile kukaa na watu kula kulala yaani hawafanyi kazi zozote za nyumbani kwa mfano kuchota maji ni inshu,kufua ni inshu yaani watu wapo nyumbani kutwa lkn mm nitatoka kazini nikirudi kama nguo zangu chafu zpo nyingi inanibidi nifue,kunyoosha yaani hapo nimemtafuta mtu wakuwa anakuja kuninyooshea na namlipa hela na watu wapo hawana kazi yeyote.

Tulianza hivi...


Wakati tunaanza urafiki wetu na siku nilipokwenda nyumbani kwa mume wangu kumtembelea nilikuta nyumba inawatu wengi sana
na nilimuuliza hv ukija kunioa hawa wote nitaishi nao?yeye alinijibu hao wanapita tu hawatakaa hapa mm nikamwambia sawa lkn siku zilivyokuwa zinazidi kwenda sikuona dalili ya hao watu kuondoka hapo bado hatujafunga ndoa ikabidi nimueleze mama yangu mzazi mama akanieleza mimi niendelee na hayo mahusiano yangu alichosema yy ni kuwa watu wenye familia kubwa huwa wanajitahidi kutafuta sana.Nikaendelea hvyo hvyo  lkn moyoni mwangu sikuwa na furaha wakati huo ninaishi na wadogo zake 5 wakike 3 na Wakiume 2 na wakati huo walikuwa wakisoma shule ya msingi hadi leo wengine wamemaliza form 6,mwingine alipata ujauzito akiwa likizo ya kumaliza std 7 na kaka yake akakasirika akamtimua nyumbani na kurudi musoma,mwingine ndo yupo form 4 sasahv lkn nae pasua kichwa alipata ujauzito na ndg zake wake wakamtoa ili angalau amalize form 4 mwingine huyu ndio balaa nafikiri kiakili hayupo sawa yupo form 2 sasahv lkn mambo anayoyafanya ni balaa kwanza ni mwizi ndani anaiba hela,chupa za soda
kunakipindi alishauza kreti 2 za soda na bia 1,anavuta bangi anajidunga sindano anabani cd za ngono anakuja nazo nyumbani na anaangalia na still bado ninaishi nae hadi leo hii hv huo ni UVUMILIVU WA AINA GANI NILIONAO?

Mimi ninawatoto wadogo na sijui uwanajifunza nn?So siku zikaenda na tukaona na siku natoka hnymoon narudi hm nyumba ilikuwa imejaa mama wakwe 4 na hao 5 na ndg wengine na walikaa wengine ndani ya mwezi 1-2 wakwe 3 wakaondoka nikabaki na mama mkwe yaan mama wa mume wangu kwan yy alikuwa ndo ameshafika,sasa huyo mama ni full kualika watu nyumbani waje wamtembelee na wakija atawang'ang'aniza wabaki yaani hana huruma hata kdg watoto wake wanatunzwa hapo,yy na still anaita ndg wengine  niliyavumilia na nikawa naongea na mume wangu kuhusu alivyoniahidi kuwa wataondoka lkn kwasasa majibu yalikuwa tofauti na yale alinijibu sasa wataenda wapi?wewe vumilia wamalize shule na mwisho wa siku kila mtu atajitegemea from there furaha ya ndoa ilitoweka nikawa naishi kimazoea nimeshafunga ndoa tayr bac sina jinsi

yaani vitu vinanitesa sana  na hadi ndoa yangu imekuwa chungu yaani unajua nime
choka! Sana nishaurini tafadhali nifanyaje maana nahisi nimefikia mwisho.

Mama Wawili

Reactions:

4 comments:

 1. Pole sana. Nakushauri Piga goti muombe Mungu wako. Baada ya mwezi mmoja kwenye tarehe kama hii ya leo njoo na majibu. Mungu wa Yakobo, Isaka na Abraham hujibu sala za kila binadamu.

  ReplyDelete
 2. Pole, wala hauko peke yako ndio familia za kiafrika zilivyo, hasa makabila yetu haya ya kutoka kanda zote za ziwa ndio usiseme. Sasa wewe ukiwa umetoka kwenye nuklia family kama familia za kichaga basi utaona shughuli pevu. Lakini kama umetokea kwenye familia za kihivyo basi hutaona shida.

  Tatizo lako mdogo wangu kabla hujaolewa ulishaweka negativity kuhusu ndugu wa mumeo basi lazima itakunyima raha katika maisha yako. Hebu ngoja nianze kuchambua moja moja

  1. Wakwe wamekuja harusini kisha wameenda zao, wewe umechukia nini?
  2. Mama mkwe anaita ndugu waje watembee huko kwenu na wabaki kutokana na attitude yako, ukichange your attitude ukaanza kupenda watu hata kutia adabu kwa style hiyo
  3. Inaelekea mumeo familia yake ndio inamtegemea na wewe umeolewa umewakuta unataka awafukuze awapeleke wapi? Kama uliona huwezi kuishi na watu ni nini kuolewa?
  4. Inawezekana wewe ndio source ya hao wasichana kuharibikiwa kwa sababu hawana mapenzi wala muongozo humo ndani. Ingekuwa ni wadogo zako wa tumbo moja na wanakutegemea wewe ungewaacha waharibike.

  5. Start changing your attitude na hata usoni utaonekana tofauti na kila kitu kitabadilika, badilika uwe mtu wa kikombe kiko half full badala ya half empty.
  6. Kuhusu kukufulia nguo si na wao wanakwenda shule au sijasoma vizuri kuwa wanasoma? Unafikiri kwa attitude uliyonayo na inaonyesha wazi kuwa huwapendi watakupenda mpaka wakufanyie kitu kama kukufulia? So long as wao wanafua nguo zao wewe shida yako iko wapi?

  7. Ushauri: Kama unaona kazi zimezidi humo ndani na wewe unachoka basi mwambie mumeo akuwekee msaidizi hata wa kwenda na kurudi aje afanye usafi, apike apige pasi, wewe ukirudi jioni unakaa kitako unaongea na mama mkwe, au unacheza na watoto wako. Wewe hao wapo temporary wa kike wataolewa wataenda zao wakati ukifika wakiume na wao itafika muda wataanza kujitegemea, waache kaka yao awasomeshe.

  ReplyDelete
 3. my dia hizo ndo familia zetu za ki africa tunaishi kwa kutegemeana na hauko peke yako mpenzi so dont feel so desparate na ndoa yako just start feeling happy na utaenjoy, hao watu ni kwel mumeo hana kwa kuwapeleka so utaendelea kuishi nao hapo mpaka hapo watakapokua na maisha yao..,jitaidi tu kuwasisitiza wasome na huyo mama mkwe kaa nae vizuri kabisa mana hujui ni kiasi gani alipata shida na hyo mumeo na ndo maana anaona hata fahari kuwaita ndugu zake waje waone anapokaa kwa mtoto wake,
  hayo ni maisha ya muda tu my dia wataondoka wote so jitaidi kuwa na uvumilivu hayo ndo majaribu ya hizi extended family tulizonazo,

  ReplyDelete
 4. Hata mimi mtoa mada sijampata; na nachelea kusema yeye ndio tatizo.

  Wewe kama unajua kuwa hupendi watu kwa nini ulikubali kuolewa na mwanaume anayeishi na ndugu zake??? Ningekuhurumia kama wangekuwa wamekukuta...ila wewe umewakuta...na usipoangalia bidada utawaacha kama ulivyowakuta!

  ReplyDelete