Wednesday, August 8, 2012

 Anikulapo Kuti akiwa na wake zake watatu wakati wa ndoa yao.

FELA Anikulapo Kuti, raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) ametoa mpya kwa walimwengu kwa kufunga ndoa na wanawake watatu.
Mtu huyo ambaye anatumia jina la mwanamuziki  aliyevuma zamani wa Nigeria, hayati Fela Anikulapo Kuti,  amefunga ndoa hiyo kufuatia mchungaji wa kanisa lake nchini humo kuwaambia waumini wake kwamba wanaweza kuoa wanawake wengi, jambo ambalo limeleta mkanganyiko mkubwa kwa waumini wa madhehebu ya Kikristo barani Afrika.
Ndoa hiyo ilifungwa kama kawaida, ambapo watu hao wanne waliapa kuwa mume na wake zake, wakishuhudiwa na watu kibao huku kiongozi aliyeifungisha ndoa hiyo akinukuu vifungu vya Biblia ambavyo hutumiwa na Wakristo wote.
Tukio hili limeleta mkanganyiko mkubwa na kuwaacha watu wengi wakijiuliza mengi kuhusu madhehebu ya Kikristo yanavyojiingiza katika matendo yasiyoendana na imani yao, ambayo inasisitiza mke au mume kuwa na mwenza mmoja tu.

Reactions:

3 comments:

  1. kikowapi??? si mlikuwa mnawacheka waislam.

    ReplyDelete
  2. Dini zimekuwa biashara...mwenye kanisa ameona akiruhusu wake wengi atawapata wafuasi kwani vigezo na masharti vimepunguzwa. Ndio maana kuna wanaotaka hata kuruhusu gay marriage

    ReplyDelete
  3. Watu watunukulie hivyo vifungu vya bible vinavyokataza ndoa ya wake wengi. Waumini wa kanisa la mitume na wachungaji wao wanaoa wake wengi tena zaidi ya wa 4.

    ReplyDelete