Monday, July 30, 2012

Dada Habari, mimi nimeolewa nina miezi mitatu sasa, mume wangu huwa anakaa london tuna rafiki mmoja ambaye na yeye yupo huko london wakati mume wangu alipofikia kutaka kuoa siku alikuwa anaongea na huyo rafiki yetu na kumueleza lakini akawa anasema kila mwanamke anayepata mama yake hamtaki kwahiyo kaishia kuwa tu na wanawake wengi lakini kuoa hakuoa, ila sasa amechoka na kwamba anataka kuoa, yule dada akamwambia kuna rafiki yake mmoja yupo Dar ni mzuri na ukimpenda sidhani kama atakataa umuoe.

Basi yule dada akanipigia simu na kunieleza mengi kuhusu huyo kaka nami nikamruhusu ampe namba yangu ya simu, kweli yule kaka akanipigia na kunieleza kama rafiki yangu amenieleza nami nikamwambia nimeshaambiwa, basi tukawa tunawasiliana, mapenzi yakaanza kwenye simu, nikamtumia picha zangu na yeye akanitumia zake, kweli nilikuwa na enjoy sana kuwasiliana naye japo hatujawahi kukutana uso kwa uso mpaka siku akaamua kuja Dar sasa, nikakutana naye alikaa kwa wiki mbili toka amerudi akaniomba anipeleke kwao Mwananyamala, kweli tulifika nikamuona mama yake na dada zake wanne na wote walinipenda sana na kumwambia aoe sasa sio kuchezeana tu.

Alikuwa akae nchini mwezi tu lakini ilibidi asogeze siku mbele baada ya kufikiria kwanini tusioane, aliponiambia mara ya kwanza nilisita kwamba hatukujuana sana alafu tu anioe, na nikamwambia kwamba unakaa mbali itakuwaje akaniambia atanioa alafu aondoke anitafutie visa nami nitamfwata baadaye, lakini atakaponioa inabidi nikakae na mama yake mpaka atakaponitumia yanayohitaji kupata visa ndio niondoke.

Basi sikuona kama ni vibaya maana kweli mama yake alikuwa ananipenda, siye ndoa zetu za kiislamu hazina maandalizi makubwa kiivyo, wazazi wangu wakaanda wakaja kunioa, tukahamia kwa mama yake na tulikuwa tunaishi vizuri sana mpaka wiki tatu baadaye mume wangu akaondoka kurudi London.

Nikaendelea kuishi na mama mkwe na wifi zangu, lakini niligundua baada ya mume wangu kuondoka wakaanza maneno kwamba wameuziwa mbuzi kwenye gunia na maneno ya uswahili kibao, yani ikafikia wakati nikiwa jikoni nawasikia nje huko wakinisema kwa mafumbo,siku mume wangu alinipigia simu nikaamua tu kumwambia ukweli kuhusu ndugu zake yeye alichonijibu ni kwamba nitakutumia hela upange chumba hata kimoja, siku niliumwa sana na wala hawakujali kuumwa kwangu nikaamua kwenda hospital kupima nikakutwa na malaria nikaandikiwa dawa nikanywa kumbe nilikuwa ninamimba changa ikatoka!!!!! maana nilitokwa sana na damu nilipomuhadithia mama mkwe ndipo aliponiambia mimba itakuwa imetoka.

Kile kitendo cha mimba kutoka wifi zangu ndio wakapata cha kunisemea kwamba nimeona mwanaume kaondoka ili niendeleze umalaya bora nitoe mimba kuliko kuwa nayo!!!! kweli mtu unaweza ukaolewa halafu kwa mara ya kwanza unapata mimba uitoe????? wakawa mpaka wanaingia chumbani kwangu na kunipekua na kuchukuwa vitu vyangu vya thamani nikimwambia mama mkwe anasema ndio wifi zako tabia zao walivyo wavumilie tu mama..kweli!!!!!!!!! 

Nikaona nyumba hii vituko haviishi nikampigia mume wangu kwamba naondoka, akaniruhusu nikaondoka na kurudi kwetu, sasa baada ya kuondoka wifi zangu wakaampigia mume wangu kwamba nimetaka kuondoka kwasababu nina mwanaume mwengine na pale kwao nilikuwa nabanwa ndio maana nimeshindwa kukaa nao na mama mkwe akamwambia bora anipe talaka simfai!!!!! mume wangu kanipigia simu ananifokea na kunitukana na kuniambia kwamba mama yake hata siku moja hawezi akamdanganya na anajuwa lililojema kwake.

Jamani ndoa haina hata mwaka misukosuko mpaka nimechoka, sasa huyu mama mkwe na wanaye sijui wananitafuta nini mimi, nikiongea na yule rafiki yangu ananiambia tatizo mume wangu anapenda sana kumsikiliza mama yake na ndio maana mama yake ameshamuachisha na wanawake kibao japo hakuwaoa mwanzo na sasa anataka kumuachanisha na mkewe labda amemtoa mwanaye kafara kwamba siku zote amuhudumie yeye tu na si mtu mwengine.

Jamani kweli hii inawezekana, na kama ni kweli nikubali tu kuachana na mume wangu maana hii aibu sijui nitaificha wapi hata mwaka wa ndoa sina!!! 

4 comments:

  1. Pole binti kwa matatizo uliyonayo, tabu ya kuolewa na familia za kimasikini ndio hii, watu wote wanakaa kitako kumsubiria mtu mmoja. Na inaonyesha hao wifi zako hawana shughuli za kufanya maana wangekuwa busy na shughuli zao wasingejishughulisha na mke wa kaka yao.

    Kuhusu mimba kutoka ni hivi, sio lazima itoke kwa dawa za malaria, hiyo itakuwa ni stress tu ndio imekufanya mimba ikatoka. Nakushauri anza process za kwenda kuishi na mumeo, usikubali kufanywa mke wa Bongo wakati mume anatanua huko Ulaya.

    Kikubwa zaidi funga siku 7, na usiku uamke ufanye sala za haja umuombe Mungu akufanyie wepesi ili kwanza mumeo aujue ukweli, pili akufanyie mipango ya safari uondoke, maana usipokazana hutaenda kwa mumeo. Vitabu vya madua vinauzwa madukani vimejaa tele, nunua uwe unasoma. Kisha usali sana maana hiyo familia wanaona ndugu yao akiwa na mke ndio itakuwa mwisho wa kuhudumiwa. Ukiweza baada ya sala ya ijumaa soma ayatulkursiy x 70 kwa ajili ya kinga na umuombe Mungu akufunguliye mambo yako, kama hii ndoa ina heri na wewe utaenda kwa mumeo kama hakuna basi itaishia.

    Kingine kuhusu aibu sio wewe utakayepata aibu isipokuwa huyo mwanaume na nduguze!

    ReplyDelete
  2. Yaani dada kwa ushauri wangu mm naomba kaa utulie usiwasikilize hao mawifi na huyo mama mkwe ambaye anataka mwanaye awe ndondocha wake, ww usiumize kichwa sana msikilize huyo mwanaume anasemaje na kama naye mwanaume anaungana na mama yake achana naye kuachwa au kuachika na kuolewa au kuoa yote hupangwa na mungu unaweza kuta mungu hakuipanga ndoa yako na atakuja kukupangia mpaka mwenyewe ukafurahi, huyo mama mkwe ni mwanga kamfanya mwanaye ndondocha wa nje tulia msikilize mwanaume anasemaje pole my dear . Grace wa Kimara

    ReplyDelete
  3. my dia we sio wa kwanza kuachwa wala kuachika wala usijisikie vby kihivyo kwanza ni bora umerud nyumban mana ungeendelea hapo ndo ungepigwa kabisa na hao mawifi na mama mkwe,cha msingi sahiv we tulia tu nyumban na mume kama ana akil ataongea na wewe vizuri na kujua chanzo ni nini mume akikutaka ukaishi nae we nenda ila kule kwa wakwe usirudi tena ulifanya makosa sana kukubali kukaa kwa wakwe ungejua mapema ungepanga chumba chako kuliko kukaa ukweni

    ReplyDelete
  4. shoga pole sana,najua uchungu unaopata sababu nimepitia ndoa kama yako.niliolewa na mume wangu ye akiwa uk mi niko bongo ndoa ikapitishwa bahati nzuri niligoma kuishi kwa wakwe nikaendelea kukaa kwetu kule mume wangu akiendelea kunifanyia mipango ya safari.ila mkwe wangu na na wifi walifanya ya kuyafanya safari kila ikikaribia kutiki gfla mambo yanaharibika masimango kila siku japo nipo kwetu!nikifanya jambo dogo mumu wangu anapigiwa simu loh.nilivoona safari kila siku inagoma nikamshauri mume wangu arudi kwani maisha ni popote iyo ilikuwa baada ya mwaka mmoja na miezi kadhaa nilivumilia yote shoga angu.nashukuru alinisikiliza mie badala ya nduguze na akarudi sasa ivi tuna miezi kama 10 na maisha yanaendelea vizuri.so uvumilivu unahitajika

    ReplyDelete