Friday, June 15, 2012

Tamaa yangu imekuwa balaa langu 2

Wapendwa wangu nadhani mtakuwa manaikumbuka hii mada niliandika siku zilizopita ninaiandika tena leo kuwapa habari  yule dada alikuja kupokea simu yake siku moja aliyopigiwa na anayetakiwa kuwa msimamizi wa kiume wa ndoa yao na kupanga wakutane.

Wakakutana siku moja ya katikati ya wiki hii inayoishia leo, wakaongea yule bestman akamuuliza shosti yapi yaliyokuponza mpaka ukaamua kuvunja uchumba na kukataa kuolewa, yule dada akawa anaongea kwamba anashangaa mchumba wake alivyokuta ile message kwenye simu yake na kukasirika wakati yeye mara nyingi alikuwa akienda kwa mchumba wake anakuta vitu vibaya tena vya kumuumiza roho lakini kila akikasirika akiombwa msamaha anamsamehe anasema mara alishawahi kuenda zaidi ya mara mbili akakuta condom zilizotumika pembeni ya kitanda wakati wao hawatumii condom.

Alipomuuliza mchumba wake akajitetea akamuomba msamaha baadaye akasamehewa, ukiachana na hayo na maudhi tu mengine madogomadogo anayoyafanya marakwa mara na kusamehewa kwahiyo ilivyotokea yeye kukamatwa na ile message na kutaka kupigwa akagundua kumbe mkuki kwa nguruwe na akaona kwamba ni heri akatae mapema kwasababu yule kaka hakuwa na moyo wa uvumilivu na subira kutaka kumuuliza na kujuwa ile message ilikuwa ya nani yeye kakurupuka tu na kutaka kumpiga.

Basi yule bestman akaaza kumpa ushauri yule dada kwamba hakuna mahusiano yenye mteremko tu na mahusia mengine kibao, baadaye yule dada akaanza kulainika na mwisho akaulizwa kwahiyo unataka kuolewa ama ndio hutaki tena ndoa yule dada akasema yupo tayari kuolewa lakini wakae kwanza na mchumba wake waongelee matatizo yao.

Basi ikapangwa siku wakakutana, na bestman akiwa kati yao wakaongea na kufikia muafaka wakusameheana, sasa basi yule kaka akasema inabidi tena tuite watu tuwaeleze haya na kwamaba tuendelee na vikao pande zote mbili, na inabidi sasa waanze tena kutafuta kumbi ya hiyo siku yao ya harusi maana shosti alivyokataa kuolewa jamaa alianza cancelling vitu vyote ambavyo vilikuwa vimelipiwa.

Haya tunawatakia maisha mema na ndoa yenye baraka tele.

Reactions:

3 comments:

  1. kila la kheri,, hakuna mahusiano yasiyo na kero na matatizo ni kuzoea na kujiheshimu wew kama mwanamke

    ReplyDelete
  2. ASANTE SANA DADA ROSE KWAKUTUJALI MAFANS WAKO UBARIKIWE KWAKUTUJULISHA KINACHOENDELEA NA HIYO COUPLE IMEKUWA VIZURI KAMA MUNGU AMEMGUSA HUYO DADA AKAKUBALI KUKUOLEWA NA HUYO KAKA NI KUWAOMBEA TU ASIJE TENA KUBADILIKA NI VIZURI TUMESIKIA UPANDE WA PILI YA SHILINGI MAANA SAA NYINGINE HUWEZI JUA MWENYE KOSA NI NANI NIMPAKA UJUE KILICHOWASIBU WOTE UBARIKIWE DADA ULIYEBADILISHA MAAMUZI YAKO NA WEWE KAKA POLE KWA MAJARIBU LAKINI MUNGU AKIWAJALIWA MMALIZE SALAMA HARUSI YENU MKAE MMALIZE TOFAUTI YENU MAANA SIKU ZOTE SHETANI HAPENDI MAHALI PENYE MAFANIKIO MUOMBE MUNGU SANA AWATANGULIE NA HILI GOOD LUCK NAWATAKIA HARUSI NJEMA UBARIKIWE NA WEWE DADA ROSE ENDELEA KUTULETEA MAMBO MAMBO MAZURI KWANI TUNAJIFUNZA MENGI KUPITIA HII GLOB YAKO NAIPENDA SANA

    ReplyDelete