Thursday, June 14, 2012

Alonalo kajaaliwa...(Chokoza shoga yangu wewe..)

Jamani leo kuna mtu kanikera eti anataka kunirusha miye roho utamrusha nani roho wewe wa kuja dar mwenziyo nimezaliwa hapahapa, hayo uliyojifunza wewe kutaka kunichamba miye mimi niliimbiwa nilale tokea tumboni mwa mama yangu..shaurilo moto huu gusa kwa utaratibu utakuunguza

Mshamba wewe jijini hapa umeshaanza kujuwa vibwana wamekutatua marinda umepata visenti unajuwa kuvaa na kukesha disco unajiona umefikaa!!!!! unadhani wewe ndio wa kwanza kuwa na mume wa mtu mpaka ujitape kama umeona chiii uvunguni mwa kitanda wenzio hizo zilikuwa zilipendwa ndio maana leo tunao nyumbani wewe umri unaenda mpaka leo huna wa kukuweka ndani kumyima mtoto wa watu raha unamdanda mumewe kila kukicha ungekuwa mzuri si ungepata na wewe wa kukuweka ndani kwanini uibe wa mtu.

Wewe unamchukuwa mume wa rafiki yako??? unajitongozesha kisa umeona kijana ana hela basi wee ukimuona tu chini kote kumejaa maji nyoooo, unadhani mwanaume akitakwa anakataa kakupa huondoki unataka kung'ang'ania halafu unakaa naye mpaka asubuhi haya shoga yako akiwa analia na kukonda kuhusu mumewe unamuhonea huruma kumbe moyoni unamg'onga MANINA zako wewe.

Juzi unaonekana hotel fulani na mumewe mtoto wa watu aja ambiwa analia mpaka anazimia akifa utamla nyama???? ngoja apone vizuri manina zako tutakuonyesha wewe. mtu akikaa kimya unamuona mjinga???? lione gumegume lenye nuksi hakuna anayekutaka kukuweka ndani umezalishwa na kuachwa unatafuta wa kukulelea watoto kwanini usiombe msaada kwa baba zao ama ndio washakutapika wala vipya sasa iloooo waliyekuzalisha tu hawakutaki utadumu na mume wa mtu? kama angekuwa anakutaka si angehamia kwako mbona bado anarudi kwa mkewe hata kama asubuhi si ungemuamisha na vitu vyake vyote????

Sikia hii yako hiyo:

Wewe type yako ya kichochoroni ndio wanaokufaa sio type yake za chumba na varanda tena ghorofani anampandia, unajuwa kwa nini bado anarudi kwa mkewe hamuachi ana ladha tamu sana ndio maana hataki kutoka hata uende na waganga lori zima himaya yake kashafika uliliye mizimu na makafara na uchinje hata paka umechemka shosti. Alah unajifanya unalipa utafuti wako ukamweka ndani utamuezea wapi wake na carolite yako iliyodunda sura imekushuka kama unachungulia ulipotoka (unapajuwa) utaisoma...

Bandika bandika yeye ata bandua wamependana wawili wewe unajichomeka...hahahahahahahahaha

Sio kila anayevaa koti jeupe daktari wengine wauza nyama...chezea smaku utanasa shaurilo

Hiyo ni msg yako nimekutumia, maana zile nyengine siuliambiwa nimesikika nikimpa shosti maneno akuambie sasa nimekupa moja kwa moja..kwa laziada unifwate siunajuwa nilipo


Reactions:

2 comments:

  1. haswaaa. mpe mpe vipande vyakeee, atajijuuuu.

    ReplyDelete
  2. Nimekupendaje leooooo. Hakya nani nawachukia hawa magume gume husband snatchers. Kuna moja hilo Ngingi fanya kazi la Bank moja lilichuka mume wa rafiki yangu; uzuri waume zetu wanajua tu hao ni wakumalizia mihemko hawana sifa za kupendwa wala kuitwa wife. Mke alivyogundua dada kapigwa chini eti linaendelea kubembeleza, tukutane tuongee mkeo kanitishia maisha. Aaah. Ukutane na nani? Endelea na mawindo kwningine. Manina zao kabisa

    ReplyDelete