Wednesday, June 13, 2012

Mkiambiwa ugomvi Msipoambiwa ugomvi..Mnataka nini???

Katika mahusiano wivu wa mapenzi ni kitu cha kawaida lakini je unajuwa jinsi ya kuutawala wivu wako kwa mwenzio? ama umeshajiuliza mimi nikiwa na wivu nakuwaje na ninavyo kuwa kunamfanyaje mwenzangu? ama wewe ndio wale mnaojifanya hamna wivu kwa mpenzi wako unamuacha afanye atakalo na awe na watu wowote atakao bila kujali madhara yake baadae..

Sikia Hii..

Kuna couple moja ni wapenzi tu walikuwa mbioni kuoana lakini waliishi nyumba moja kama mke na mume, pande za Ubungo huko, mwanaume alikuwa anamarafiki wa ajabu kweli ambao wao starehe ndio kila kitu ulevi, wanawake ndio maisha yao wakati wote kwenye hilo kundi walikuwa na wapenzi na wengine ni wame za watu.

Tabia hii ilimkera sana mkewe haswa pale mwanaume anaporudi saa nane za usiku kila siku akiwa amelewa, yani hata mkewe kumshughulikia ilikuwa tabu, mpaka atakapotaka yeye akitaka mkewe hakunaga..mkewe baadaye akaja kugundua yule kaka anamwanamke nje alipotaka kuongea naye kuhusu hilo swala yule kaka hakutaka akawa na hasira na kuishia tu kugombana sana bila sababu yule dada akajiahidi moyoni kwamba hatakaa tena kumuuliza atakuwa tu anamchukulia poa.

Mara kwa mara yule kaka alikuwa anachelewa kurudi nyumbani, yule mama kimya haulizi na wakati mwengine yule mama alishawahi kupita bar akamuona mpenzi wake na mwanamke akaenda tu kumsalimia na akapita mume aliporudi wala hakumuuliza kitu wakaendelea na maisha, ikawa mara kwa mara yule dada anamkuta mumewe na wanawake lakini wala hakumuuliza maana alijuwa hata akimuuliza wataishia kugombana na hatimaye kupigwa kwahiyo alikuwa tu anampuuzia.

Siku moja yule dada akapata wa kumshauri kwamba utakuja kufa kwa ugonjwa wa moyo kumuwaza mumeo ili ukae kwa raha juwa dawa ya mwanaume ni mwanaume mwenziye siku zote, wala hutaumia hata ukimkuta anakumbatiwa nje, basi yule dada kwa siri naye akatafuta wa kumpooza moyo, kweli wala hakuwa na muda na mumewe na wala hakukaa kuuliza aliishi kama hakuna matatizo kwenye ndoa yake.

Kumbe mwanaume alikuwa amemuweka kiporo siku moja akaanzisha tu ugomvi kwanini siku hizi uniulizi tena kama nina mwanamke, kwa nini kitandani huombi upewe raha kwahiyo kuna mwengine anayekupa huko pembeni, kwanini wewe mwanamke huna wivu na mpenzi wako, yule dada akauliza kwanini niwe na wivu na wewe wakati nimeshakujuwa nimeamua tu kukaa kimya.

Baasi lile jibu ilikuwa kosa, unanijuwa nini lazima utakuwa na mabwana alimpigaje yule dada, piga piga na wewe akaenda akachukuwa kisu akamchana yule dada kila mahali akamchoma mpaka akafa, sasa makelele ya yule dada yakawashtua majirani wakaja kugonga hapakufunguliwa wakaamua wavunje mlango yule kaka kuona ameshaua na watu wanakuja akaamua kujitoboa na kisu mpaka utumbo kudondoka naye akafa. Majirani mpaka kuvunja mlangu na kuingia wakakuta wote wameshakufa.

Marafiki wa yule dada, ndugu na majirani ndio waliotoa hii story maana wao walimjuwa yule kaka alivyokuwa muhuni na kumtesa mkewe, maana bar Ubungo zilikuwa zinamjuwa kwa totoz.

Kuna msemo unasema kuku wako mwenyewe manati ya nini? kurudi mwenyewe bandani haitoshi kuhashiria anaijuwa nyumba yake, mapenzi yanahitaji umjali, umthamini na afurahie kurudi nyumbani kukutana na wewe tena.


2 comments:

  1. Da!inasikitisha kweli. May their souls RIP

    ReplyDelete
  2. haya ndo mapenzi ya siku hizi, kiukweli ni siku z mwisho ndoa zimekuwa chungu mapenzi hakunaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa kabisaaaaaaaaaaaaaa.

    ReplyDelete