Monday, June 18, 2012

Unaichezea ama Inakuchezea...

Leo nataka kuongelea pesa kwenye nyumba, tunajuwa ya kwamba mwanaume unapoamua kuoa inamaana upo tayari na unajikimu kujitunza na familia yako pia ambayo unategemea kuianza lakini kwa vile sasa maisha ni magumu na yamebadilika inatufanya na sisi kina mama kufanya kazi kutafuta hela kusaidia familia na pia kuweza kujikimu wenyewe maana kuna wame wengine bwana ukimuomba hela basi atanuna yeye anaona jukumu lake ni kulisha tu nyumbani na kusomesha watoto mke kumtunza sio lake kabisa ukiwa kama mama huna hela utambuka hapa mjini.

Unanuna nini sasa hutaki mkeo akapendeza, akavaa akaonekana kweli mke wa fulani hapana chezea ni mzuri anapendeza ama nyie ndio wale wanaume mnaopendezeshewa wake zenu unamuona mkeo anang'ara unajitapa kwa wenzio mke wangu ni mzuri sijui anapendeza hujiulizi hana kazi hela za kujipamba katoa wapi...ama hujiulizi sijawahi kumletea mke wangu hata kanga akavaa akapendeza ama pochi akabeba akaonekana barabarani..hujiulizi hilo!!!


Sikia Hii...

Kuna dada mmoja aliolewa na wakawa na watoto wawili, mumewe hakuwa na kazi ya kueleweka kama mke wake kwahiyo majukumu mengi nyumbani mkewe ndiye aliyeyatetua, kuhusu mapenzi yalikuwa tu yakawaida maana siunaelewa mama akiwa anaingiza hela kuliko baba basi mwanaume anaona vibaya kazi yake kushinda kwao na kupewa maneno kibao ya kuvunja ndoa yao, anaambiwa kama anauhakika hizo hela za mkewe ni kazi tu ama mkewe anakidumu pembeni kinamsaidia na mengine mengi si unajuwa tena maneno ya mkosaji.

Basi yule kaka akaanza madharau tu na ugomvi tu usioisha kwa mkewe, kila mara wanagombana visa haviishi na vyote mkewe anasema havieleweki ila watagombana itafikia akisema huyo hawara yako anayekupa hela ndio anayekutia kiburi unidharau..jamani maana kashasikia hayo mpaka kayachoka.

Sasa basi yule kaka kwao waliachiwa nyumba ya urithi wakaamua kuuza na kila mtoto kupewa Millioni kumi na tano, bila hata kumwambia mkewe siku hiyo karudi nyumbani akachukuwa bag na kuanza parking nguo zake zote na kumwambia mkewe wewe siunajeuri na hela ulizonazo sasa nami nimezipata zangu naondoka tutaonana MUNGU akipenda na kufungua mlango na kuondoka, mkewe alijitahidi kumbembeleza mumewe asiondoke na kumuuliza mbona kosa halioni ila kila siku wanagombana akamwambia kweli hana mwanaume ni hela zake tu anazofanya kazi na kufanya biashara alijaribu kweli kumbembeleza akilia akimuomba muewe kuwaonea huruma watoto wanamuhitaji, yule baba hakusikia kitu akaongoza njia na kuondoka zake.

Na ndio mwisho wa kumuona mumewe miezi minne ikapita akakutana na rafiki wa mumewe siku moja na kumueleza mumeo mbona yupo Dar hii hii anaishi na mwanamke kariakoo, kazi yao kutanua tu na kubadilisha hoteli kila siku roho kweli ilimuuma lakini atafanyaje basi akawa tu anaendelea na maisha yake.

MUNGU alivyowaajabu mwezi baadaye anaona simu inaita namba haijui kupokea sauti anayoifahamu ikamuitikia hujambo mke wangu? za masiku nimekukumbuka sana, anasema alivyosikia tu vile akakata na simu hakutaka kuongea naye kabisa, baada ya siku mbili mumewe akarudi nyumbani anaomba msamaha na kulia kama mtoto kwa jinsi alivyokosea familia yake na kumuomba mkewe amrudie tena kwani shetani alimponza na wivu wa mapenzi ulimtawala hakujuwa la kufanya zaidi ya kuondoka baada ya kupata hela.

Mkewe anasema yani hata hamu ya kumuangali usoni alikuwa hana, akamuuliza kwahiyo hela ulizopata zikowapi akamwambia sina hata shilingi mke wangu, sijui nilizitumia vipi mpaka zikaisha ila tu nilinunua pikipiki moja na kumpa mtu awe ananiletea hela mwisho wa wiki 50,000/= nitakupa mke wangu uwe unaisimamia wewe na hela uchukuwe wewe nisamehe mke wangu...hayo ndio maneno yaliyokuwa yanamtoka jamaa.

Akamuuliza kuhusu hiyo story aliyosikia kuwa alikuwa na mwanamke kariakoo kazi yao kuzunguka tu mahotelini wala hakukataa akamueleza ni kweli na kuendelea kusisitiza kuomba msamaha na kumsisitiza mkewe awaonee huruma watoto wasije kuishi bila baba yao na maneno mengine kibao..

Mkewe alichokifanya ni kumfukuza tu yule kaka, maana hata nyumba si alikuwa analipa mwenyewe akamwambia ampe muda afikirie la kufanya halafu atamtafuta, yule kaka wala hakuondoka analala barazani kila siku akingojea msamaha wa mkewe, akiamka anakaa tu hapohapo barazani watoto wake wanakuja kukaa naye ikifika mida ya kula wanaingia kula dada anampelekea baba chakula nje usiku analala barazani, mkewe anasema wala hamuonei huruma ukilinganisha na alichomfanyia anayewaonea huruma ni watoto ambao lazima wakakae na baba yao nje mpaka wanapotaka kulala ndio warudi ndani.

Anasema roho yake inamuuma sana hata akimsamehe anaogopa asije akapata tena hela na kuamua kuondoka tena, hamuamini tena na anasema hata akiamua kumsamehe hadhani kama ataweza kuishi naye kama mwanzo kwa mapenzi...

Wewe mwenzangu unaona hili ni jema, ama afanyaje?
Reactions:

5 comments:

 1. DUH! ASNTE DADA ROSE KWAKUTULETEA KISA JUU YA KISA UBARIKIWE SANA HII BLOG YAKO NAPENDA MAANA KILA LEO UNATULETEA MAMBO MAPYA NA TUNAJIFUNZA MENGI KUPITIA HII BLOG YAKO ASAS NAKUJA KTK USHAURI WANGU NAFIKIRI HUYU DADA ITABIDI ARUDISHE ROHO KWAKUWA TU WEMECHANGANYA DAMU NA HUYU BABA WAMEZAA WATOTO AITISHE KIKAO YA FAMILIA YA PANDE ZOTE MBILI NA WASHENGA NA WATU WA DINI PIA WAKAAE CHINI AEKEZE KILA KITU NA AKISHAONYWA AMPE MASHARTI ILI ASIJE TENA KURUDIA KITU KAMA HICHI NA PIA AKUBALI WAKAPIME DAMU KICHEKI AFYA YAKE AKISHAKUBALI HAYA YOTE HANABUDI KUMSAMEHE KWANI AKIMFUKUZA NA WATOTO WAMESHA MZOEYA BABA YAO ITAKUWA TABU KWA WATOTO WAKE MIMI USHAURI WANGU NI HUO TU

  ReplyDelete
 2. MM NASHANGAA MWANAMKE AKIWEZA KUHUDUMIA FAMILIA BASI ANAKIDUMU!!!!!! HUYO DADA KWAKUWA ANAWAPENDA WANAE BASI AMPE TU CHUMBA KIMOJA HUYO EX WAKE WALAU APATE JISITIRI NA WATOTO WASIMUONE MAMA KATIRI. ILA KIUKWELI HAFAI KUWA MUME KIMEO TOSHAAAAAAAAAAAAAAAA

  ReplyDelete
 3. sio wa kusamehewa kama mume..ni wa kusamehewa kama mzazi mwenzie..na kama alivyosema mchangiaji mwenzangu, kama nyumba ni yao ina nafasi apewe chumba cha kuishi humo, na pia masharti juu ili akikiuka na kuwa kero kwa mama akusanyishwe kilicho chake aondoke upesi..akafie mbele...pumbavu kabisa! yani hawa viumbe wanaboa..hawabebeki kabisa!

  ReplyDelete
 4. Kwakuwa amezaa naye watoto, na bado ni mume wake mi naona amkaribishe ndani ya nyumba na kumpa chumba. Huyu mwanaume kashakiri makosa na mpaka kuamua kulala kibarazani naona anajuta sana hayo aliyoyafanya. Dada pia kwa upande mwingine ameumizwa...ila mi namshauri amsamehe ili aweze ku-clear concious yake. Yaani hapa inabidi amuombe Mungu ampe moyo wa huruma ili aweze msamehe.Maisha ndo yalivyo jamani, kuna ups and downs. Wapendwa embu kaeni na kutafakari kama Mungu angekuwa anahesabu maovu yetu nani angesimama mbele yake?

  ReplyDelete
 5. jamani ushauri wote wa huko juu ni mzuri mimi ninatafakari hivi kama kisa hiki kingekua ni MKE- Yaani ni MWANAMKE ndo kafanya mbwembwe hizi hivi ni mwanaume gani angemhurumia na kumrudisha!!! hata kumpa chakula na kumruhusu akae barazani???? sisemi asimsamehe ila inanuma iwape we mwanamke ukifanya jambo dunia nzima itakukalia kooni akifanya mwanaume ohhh msameheni....Martha G.

  ReplyDelete