Friday, June 29, 2012

Nimeingia choo cha kike na pakutokea SIPAONI..

Siku ya kwanza nilipokutana na mke wangu nilidhani nimeona malaika yani wakati hule sikuona msichana mzuri, na aliyenivutia kama yeye sikuchelewa kwenda kumtongoza na baada ya kunipiga chenga za hapa na pale mwishoe akanikubalia na kuwa mpenzi wangu.

Kila mtu aliishi kwao kwa wazazi kwahiyo tulionana tu mtaanai na kuspendi naye kwenye mahoteli kweli tulienjoy sana wakati huo, mwaka mmoja baadaye tukaamua tufunge pingu za maisha basi mikakati yote ikaandaliwa na MUNGU akatusaidia tukaoana, wazazi wangu walinipa nyumba mbezi basi miye na mke wangu tukahamia huko.
Tukamaliza mwaka wa ndoa baada ya mwaka wa ipi mabalaa yakaanza, siku kaamka tu akagoma kuanza kunihudumia, yani kufua nguo zangu hataki nikimuuliza ananiambia hataki tu kufua nifue mwenyewe mwaka wa tatu huu sasa unaelekea mke wangu hajawahi kufua nguo zangu yani kila jumamosi nifue mwenyewe ama nimtafute mtu nimlipe anifulie, sasa tunamtoto mmoja anamiaka miwili na nusu ameanza chekechea anashinda huko mpaka jioni, mke wangu akaamua kutafuta kazi jioni akitoka ampitie mtoto ndio warudi nyumbani.

Yani mke wangu hajui hata kujituma nyumba usafi inafanywa mara moja kwa wiki hiyo ni jumapili ndio haendi kazini kwavile jumamosi mimi siendi kazini inanibidi nibaki na mtoto nyumbani na chakula nipike mimi labda niamue kufanya na usafi, ninachoshangaa mdogo wangu naye ameoa na hawana msichana wa kazi lakini mkewe anaamka asubuhi sana na kufanya shughuli zote za nyumbani mpaka wakienda kazini na mtoto shule nyumba ni safi yani mpaka namuonea wivu, siku nikamtuma mke wa mdogo wangu kwenda kuongea na mke wangu kuhusu usafi nilivyorudi nyumbani nikakutwa nimenununiwa na chakula sijapikiwa nimeambiwa nikamuoe yule mke wa mdogo wangu aje ampikie maana nimeona raha kumueleza matatizo ya nyumbani kwangu.

Nimemwambia tuweke msichana wa kazi hataki ananiambia kwamba nikimleta nitaanza kumfwatilia na kumla..yani nashindwa kuelewa nini mbaya na huyu mwanamke, kuna siku mdogo wangu kaja kwangu ameshindwa kabisa kuingia ndani anasema kunaharufu kali..hapo ndipo nilipoona sasa nitaumbuka niombe msaada maana hata raha ya ndoa siioni, nakuwa mtumwa wa ndoa, hata kufanya naye mapenzi siwezi maana sina raha, siwezi simamisha kabisa hata hisia ya kufanya naye tendo sina, na yeye wala hajali wala hajawahi niomba.

Reactions:

6 comments:

 1. kwanza pole kwa yaliyokukuta.

  1. Hivi ulioa huyu mke kwa kumpenda au ulilazimishwa?? Je wewe mwenyewe huwa unamsaidia shughuli za nyumbani ukizingatia hamna msaidizi au sababu umemuoa basi umemgeuza mtumwa??

  2. Mwanzo ulimuona malaika sasa hivi unashindwaje kuendelea kumuona malaika?? Mpende mke wako kaka kuwa na mawasiliano ya ndani na sio kupeleka taarifa nyumba ya tatu kuja kukusaidia matatizo yako.

  3. wewe ni mmoja wa wanaoishi humo ndani, kama wife hawezi kufanya usafi na inakukera siku hizi kuna makampuni yanayofanya hizo kazi mbali na kupata kijana wa kukufanyia usafi twice a week kwa hiyo na wewe changamka. Vinginevyo kaa kimya uendelee kufurahia uchafu.

  ReplyDelete
 2. Pole sana kaka, yaani hapo sijajua ni kwanini mke wako kabadilika, Je alishawahi kukuhisi tofauti au kuna kitu alikikuta kilichomhakikishia kwamba may be unamsaliti au ulimkosea jambo kubwa. Kama sivyo basi huyo mdada ana hila zake. Mimi nakushauri ili kuweka nyumba katika mazingira ya usafi tafuta dada wa kazi awasaidie kwa kweli, uchafu nyumbani haupendezi na wageni watashindwa kuja maana nyumba itakuwa haivutii. Pili shirikisha wazazi wake maana hao wanaweza kujua wapi pa kuanzia kumkanya binti yao. Tatu usimuache Mungu, muombe sana Mungu akupe amani maana naona ndoa yenu imeshaingiliwa na pepo mchafu. Bila msaada wa Mungu upendo kati yenu utakwisha kabisa. Mungu akuongoze na umvumilie mkeo.

  ReplyDelete
 3. Napita ntarudi...akina mama akina dada mukuje hapa hili linatuhusu....

  ReplyDelete
 4. mke atakua anazidiwa na majukumu,mana mtoto bado ni mdogo jmn usiombe mtoto awe mdogo afu hauna hd au mtu wa kukusaidia inatesa sana,ndo mana anashindwa kukufulia kama zamani.

  mweleweshe vizur ili mtafute hg. kumsema kwa watu wengine haitasaidia zaidi ya kubomoa,na sio vizur siri zake kumpelekea hy mwanamke mwingine sijui ndo shemej unazan atajisikiaje?haipendez kwa kwel

  hata huyo unaemwaona bora nae pia ana matatizo yake mengine,so vitu vya nyumban ni vizur mkashauriana wenyewe.

  ReplyDelete
 5. Siamini! Mimi ni mwanamke lakini nimekasirika mpaka nakwambia "be a man!" Huyo mwanamke inakuwaje anakuendesha utadhani mwanamke wa kizungu wakati ni mbatu. Peleka kwao utakufa siku si zako. Mpeleke kwao waeleze A-Z na mwambie hauko tayari kukaa nae mpaka ajirekebishe. Mimi ni mkristu lakini maisha ni mafupi mno; till death do us part ina exceptions bana.

  ReplyDelete
 6. Yani kazi kufanya hataki; housegirl hataki. Anachekeshaaaa. Eti utammega. Wanawake mbona hatujiamini??? Mimi niko g'ambo nafanya PhD na mume wangu yuko Tz na wanangu na house girl. Mbona wala mshipa wa roho haunisumbui eti atammgegaa. Lol. Kwani mwanaume muhuni anasubiri aletewe ndani na wanawake wamejaa mitaani. Huwezi kumzuia mwanaume kuchiti bana kwa kukataa kukaa na msaidizi unless huyo mwanaume ni animal. Lol. ambaye ni full mfadhaiko. Hata hao animals kutokuwa na housegirl hakuwabadili tabia.

  ReplyDelete