Thursday, June 28, 2012

SOMO..

Leo nataka niongee na nyie wanaume, unajuwa bwana usafi asikuambie mtu ukiwa msafi utaheshimika na kupendwa pia wengi watatamani kuwa karibu yako, sasa iweje weye na hili nataka niliwaseme wanaume na wake zenu utamkuta mtu mwanaume wa maana mzuri kajaa midevu kaa beberu, looohhhh mwanaume huna hata appetite ya kuangaliwa mwanamke akikuona mpaka anataka kutapika, ebo sasa kama kidevu tu hivyo huko pengine panakuaje siunaweza suka...

Na wewe mwanamke hukufundwa wewe wakati unaolewa kwamba lazima ujuwe muda wa kumfanyia mumeo usafi sawa kidevu na nywele huwezi labda kumfanyia kwanini usimshauri akaenda kwa kinyozi kunyolewa!!!!!!!! ama wewe unapenda ukiwa kwenye sita kwa sita ukilamba koni uchomwe na hivyo vinywele maana miye hamu yote ndio itakuwa imeishia hapo...

Jamani aihusu hata kidogo kutembea kaa beberu barabarani, miye nikikuona tu hivyo midevu imekujaa mkeo marks nishamshusha maana hajui jukumu lake..ushansoma?????
Reactions:

2 comments:

  1. Hivi wewe dada unajua kuwa kuna watu wanaachia ndefu kutokana na imani za kidini na haihusiani kabisa na usafi wa sehemu nyingine za mwili? Hebu google ujue kwanini wayahudi na waislamu wanafuga ndefu usikurupuke tu kutukana watu. Kuna watu wana ndevu na ni wasafi, na kuna watu wao hawaoti ndefu usoni kwa hiyo hawana ndevu lakini ukiwaangalia makwapa yamejaa nywele kama msitu wa Kazimzumbwi. Na wengine ndevu za juu wananyoa vizuri kwa kinyozi lakini usafi wa kwingine ni shughuli.

    Kwahiyo kutokuwa na ndevu sio kigezo cha usafi na kuwa na madevu pia sio kigezo cha usafi. Kwanza kama hao waislamu kwenye mafunzo yao wanamaelekezo mpaka kuhusu kukata kucha na kunyoa nywele za mwilini, na usafi mwingine.

    ReplyDelete