Wednesday, June 20, 2012

Kuna ukweli gani kwenye hili....

Kuna jambo nataka kuuliza ambalo nataka nilielewe mwenzio anapofariki kama ni mkeo/mumeo unatakiwa kukaa muda gani mpaka upate mwengine ama uendelee na maisha na mtu mwengine? ama tunavyoambiwa mpaka kifo kitutenganishe inamaana ukifa tu then its goodbye to the old chapter and hallo to the new chapter ama inategemea na wewe mwenyewe unalichukuliaje hili jambo au kwa wale wenye vidumu katika ndoa basi kwao kunakuwa hakuna jipya ni kuendeleza tu uhusiano wao bila uwoga kwasababu aliyekuwa anawafanya waufiche hayupo tena??????????????

Sikia Hii..

Kuna dada mmoja namfahamu yeye alikuwa kwenye ndoa na alibahatika kupata mtoto mmoja ndani ya ndoa yake, lakini kwa bahati mbaya MUNGU alimpenda mumewe zaidi akafa baada ya kuugua kwa muda mfupi tu.

Tokea mumewe afariki hata mwaka wa pili haujaisha huyu dada sasa hivi anamimba ya kujifungua muda wowote!!!!!!!yani watu wamemsema sana na hata ndugu zake wengine walipogundua anamimba wakamtenga, wanasema alipaswa kuenzi kumbukumbu ya mumewe kwa muda mrefu kidogo kabla ya kupata mwanaume mwengine na mpaka kuamua kumzalia!!!!

Je hili ni sawa? kuna mama mmoja yeye anasema alikaa miaka kumi ndio akaamua sasa ni wakati wa yeye kuwa na mwanaume mwengine, mjane mwengine anasema tokea mumewe afariki hajapata moyo wa kuwa na mtu mwengine kwani anahisi bado anamsaliti mumewe!!!!

Labda hawa ni wamama wa zamani ndio wanajiheshimu kihivi na kuthamini wame zao hata wakiwa hawapo, maana ndoa za siku hizi wame/wake wapo lakini pembeni kuna vidumu zaidi ya vitatu je sasa huyo mumeo/mkeo akifariki utafanyaje?????????? uchungu wa mke/mume utakuwepo au wale wapembeni ndio watakuwa bembelezo lako na kutojali kabisa pengo aliloacha mwenzako?????

2 comments:

  1. watu nao,wamtengee nini jamani?kwa kuwa kiatu hujakivaa wewe kwa mwenzako unaona ajabu.au kwa kuwa ni mwanamke?maana wanaume wengine,wakifiwa baada ya miezi 6 tu,wanaoa mke mwengine,kisa wanasema hawataki kuzini.na hawawezi kuishi bila sex,imagine huyo mke mmejuana saa ngapi mpaka ndoa ya chap chap.mimi nahisi kila mtu anajua ku deal na jambo lolote linalomfika,binaadamu tupo tofauti.watu watasema,mwisho watanyamaza

    ReplyDelete
  2. Sasa kuna ubaya gani huyo wa miaka kumi ni muongo kama hapigi punyeto atakuwa na mtu wake anayempoza.

    ReplyDelete