Jamani hivi huku tunapoelekea kunani haswa maana sielewi, kweli usawa huu wewe mwanaume mzima umeoa halafu mama yako anakushika kichwa na kukuambia la kufanya hata kama sio sahihi kwasababu ni mama yako unamfanyia mkeo, ila angekuwa yeye ndio kaambiwa na mama yake la kufanya kwa ndoa yenu basi nyumba ingewaka moto, kwa matusi na kupigwa ama hata kufukuzwa ebo..
Rafiki yangu amenihadithia matatizo yake na nikampa ushauri na akaniomba pia niweke humu ili apate ushauri zaidi ya nini la kufanya maana mama mkwe wake anaibomoa ndoa yake, yeye yupo kwenye ndoa mwaka wa tisa huu na wanawatoto wawili wakubwa tu wenye kutambua mambo.
Huyu dada na mumewe wameihi miaka hiyo yote kwa furaha na upendo japo tunatambua mikuruzano ya hapa na pale lakini penzi lao lilikuwa imara, wanapokaa sio mbali na nyumba ya wazazi wa mwanaume, kwani baada ya kuoa wazazi wa mwanaume wakaamua kumpa mtoto wao nyumba yao iliyokuwa karibu na kwao, mwanzo kila mtu alimuheshimu mwenziye japo walikuwa wanakaa majirani sana.
Mpaka wakapata watoto sasa ananiambia mwaka jana ambayo ndio walikuwa na miaka nane ya ndoa yule mama mkwe akamuita mwanae nyumbani siku moja na kumshawishi mwanaye kuoa mke mwengine yani kwakuwa dini yao inaruhusu aoe mwanamke wa pili, na kwakuwa anajiweza kutunza familia, yani hivyo tu bila sababu ya msingi yeyote.
Mume wake kwa akili zake za kumsikiliza mama yake akaubaliana na mama yake, bila kumwambia mkewe, basi mama mkwe akamtafutia mwanaye msichana akamleta pale nyumbani kwake sasa (kwa mama mkwe) yule dada akawa anakaa pale, kwahiyo mume wa shosti kabla hajaenda kazini anapita na akitoka kazini anapitia kumuona mkewe mpya.!!!!!!
Mara kunakipindi akaanza kumuhisi mumewe kama anabadilika, anakuwa mwenye hasira (kitu kidogo tu anakasirika, mara hela haachi nyumbani, anachelewa kurudi na wanakaa hata mwezi hamjui mumewe) yeye akawa anahisi labda anamwanamke akiwa hajui mwanamke mwenyewe yupo kwa mama mkwe zile tabia za mumewe zikawa zinamkera siku akaamua aende kwa mama mkwe kupata ushauri.
Salaalaaa, alijutaje kwenda ile kufika tu mama mkwe alikuwa amekaa na yule dada wanapika akajisemesha kwa dharau kumwambia yule dada wewe ndio mwanamke wa kuwa na mwanagu sio wengive vimbaombao sijui viliokotwa wapi (na kweli akijiangalia yeye mwembamba) ndio akashtuka kama kaamshwa usingizini kumbe mume wake kubadilika akaijuwa sababu).
Mbele ya mama mkwe alienda na kumkunja yule dada, mama mkwe akawa anamshambulia akimtetea yule msichana, basi ikawa vita, maneno mpaka ikafikia akawa anamtukana mama mkwe na kumwambia maneno makali ambayo leo anajutia anasema ilikuwa ni hasira.
Akarudi nyumbani akalia sana wazo likawa moja tu kichwani aondoke, basi kabla hajaondoka ma mumewe akatia maguu, loooh walivyogombana hamna tena na haitotokeaga, anasema hawajawahi kugombana kama vile mpaka mumewe akampiga na kuondoka, watoto wakamuomba mama yao aiondoke wakalia sana basi yule mama akaamua asiondoke lakini hata lala tena chumba kimoja na yule baba.
ukapita mwezi wa sita baada ya vurumai, mara yule dada aliyeletwa na mamamkwe siku akafunga safari kwenda kwa shosti, na kuanza kumuomba amsamehe, hamtaki tena yule mwanaume aliambiwa kwamba anahela atakufanyia vitu kibao ukikubali kuwa naye sasa siku zinaenda hajaona lolote la maana analolipata, amekaa tu hata akiomba hela ya kufanya biashara kila siku anaambiwa keshokesho, sasa kaamua kuondoka hamtaki tena mumewe akaomba msamaha na kweli yule mwanamke akaondoka.
Tokea ule ugomvi kwa mama mkwe hajawahi kukanyaga, na mwezi wa sita sasa hajalala na mumewe, na anasema hana hata hamu naye maana kila akimuona hasira zinampanda na kukumbuka aliyomfanyia, anaishi tu sababu ya watoto, tokea yule msichana aondoke anamuona tu mumewe nyumbani mapema anajichekesha naye kama anataka kuleta zile za baby come back.
Anachotaka ushauri ni kwamba mpaka sasa ndoa yake haina amani, sawa ya mumewe atayamaliza hao wakwe ndio anaona aibu, japo walimkosea nani wa kumuomba mwenzake msamaha kwasababu yeye anaona kakosewa na yeye kawakosea wakwe, na hata kama akienda kuwaomba msamaha bado atawaona wanafki na mapenzi kwao tena kama zamani kutakuwa hamana maana hatakuwa nao tena karibu na heshima aliyowapa imeshaisha sasa itakuwaje kwa yeye na mumewe? je kama wewe ungekuwa mumewe ungechukuwa hatua gani? na kama wewe ungekuwa wakwe ungefanyaje? na yeye mke afanyaje?
jamani! unajua sisi wanawake tunajikuta kwenye vifungo vya maisha vya ndoa kisa watoto! sisemi kwamba eti uache wanao uondoke bali nasema hao watoto wakiishi katika ndoa ambayo inamatatizo wataathirika vilevile. Cha msingi, tunapaswa tuwe huru kiuchumi ili tuweze kuwalea watoto wetu kwa hali yoyote ile pindi ndoa ikifeli. kwani ukiwa huru kiuchumi ukiachana na mumeo utaweza kuishi kwa furaha tena zaidi kwani kero katika ndoa inakufanya mtu uone bora uwe singo! sasa kuna mana gani kung'ang'ania ndoa wakati huna amani wala furaha? na kuhusu issue yako na wakwe na mumeo, nadhani hapo mapenzi yamejaa unafki na chuki. mama mkwe wako is back stabber na usipoangalia kama nia yake ya kumtafutia mke mwanawe haikutimia, she wont rest until she finds one!!! so, to me it looks like u have to get prepared for the worst! pray for God's protection plus if you dont have a dime in ur name, u better start thinking abt finding a job or business to make u financially independent. hakuna kitu njema kama mwanamke kuwa independent. wengi tunajitesa na kukubali mateso ya ndoa kwa vile hatuna uwezo wa kusimama sisi kama siSi! ni hayo tu. DOREEN
ReplyDeletewell said Doreen,thanks so much.
DeleteMhhh jamani ndoa hizi kwakweli wanawake tunashida, Mimi napenda kumshauri huyo dada amtafute mshenga au mtu wa karibu ili waende kwa wakwe akaombe msamaha ili aweze kuishi tu na mume wake hii yote ni kwasababu ya watoto, ila wangekuwa hana watoto ningemshauri aende kwao akapumzike ridhiki ipo popote
ReplyDeleteGrace wa Kimara