Monday, February 13, 2012

SIKUPENDA ILA MAMA NDIO CHANZO..

Dada Rose, kwanza nakushukuru kwa kuwa muwazi kuweka mada katika blog yako zinazohusu mashoga, ndio najuwa serikali yetu inatutenga lakini sisi bado ni watanzania na nibinadamu tunahitaji upendo wa dhati kwa hilo dada kweli nakushukuru.

Mimi ni shoga, na sikuzaliwa hivi ila mama yangu ndio chanzo cha mimi kuwa hivi, wakati nikiwa nakuwa niligundua ya kwamba mama yangu hakunipenda kabisa, yani mpaka nikawa nahisi labda mimi sio mtoto wake, huku nikikuwa nikawa nafanya utafiti wangu kwa ndugu na wote walinihakikishia kuwa yule ni mama yangu mzazi lakini sijui kwanini hakuwa ananipenda kabisa.

Kunakipindi alikuwa anaongea na rafiki yake kuhusu mimi nikamsikia anasema hata siku nikifa atanunua kreti la bia anywe afurahi, kwakweli nilijisikia vibaya sana na nikaamua kutoroka nyumbani kutafuta maisha kuliko kukaa na mama yangu asiyekuwa na mapenzi nami.

Ndipo nilipoondoka, nikawa natangatanga mitaani, mara nikapata kazi ya kubeba zege, siku moja ya weekend nikiwa natembea barabarani ikajagari na kupaki mbele yangu kukawa na mwanaume mbaba tu sio mtu mizma saana akaniambia kwamba nimuelekeze sehemu moja hivi alikuwa anataka kwenda hakupajuwa, ndipo akaniomba niingie naye kwenye gari nimpeleke nami kwakuwa sikuwa na pakwenda basi nikaenda naye.

Mara nilipompeleka pale akaniomba niingie naye japo tukanywe soda, nami kwavile hela sina nyingi na nina njaa nikaamua kwenda ili japo siku ipite nikiwa naye na maongezi anayoongea nikagundua ni mtu wa kula wanaume wenzake, tulipomaliza akaniuliza nakaa wapi anipeleke nikamuonyesha alipogundua nakaa mitaani alisikitika sana, akanipeleka kwenye nyumba ya wageni na kunilipia siku hiyo na kuniambia kesho angekuja kunichukua anipeleke sehemu ya kukaa.

Kwa mara ya kwanza tokea nitoke kwa mama yangu nimelala kwenye kitanda na kuoga na kula vizuri, nilitumia muda huo kiuhakika, mpaka asubuhi akaja akanipeleka kinondoni akanipa chumba na sebule nikae kilikuwa kitupu hata godoro hakuna lakini nilishukuru kwakuwa nilikuwa na sehemu ya kukaa, cha kushangaza zaidi akanipeleka shopping akaninunulia kila kitu nilichohitaji na kuniachia hela nyingi tu ya matumizi japo hakunitamkia kunitaka kimapenzi nikajuwa labda ameamua tu kunisaidia hata kama nilishamhisi ni mtu wa kula wanaume wenzake hapo na biashara za zege zikawa mwisho niliona kama zali.

mpaka baada ya mwezi huku akiwa anapitapita mara moja moja kwangu na kuhakikisha nipo sawa, siku moja akaja usiku akakaa mpaka asubuhi tukiwa wote ndipo aliponitamkia hayo maneno kwamba yeye yupo hivyo kama nilivyomhisi, basi na nilikuwa sijawahi kufanya mapenzi na mwanamke kwahiyo nilikuwa sijui nanikiangalia huyu baba kanifanyia mengi na mama yangu hanitaki, huyu baba amenipa maisha mazuri ambayo mzazi wangu hakunipa nikakubali nikampa.

Kwakweli mpaka sasa ndio maisha yangu hayo nipo na yule baba na ananitimizia kila kitu na nyumba kanijengea, nina gari na tunaendeleza tu mapenzi, hapa kati mama yangu akanitafuta kwa vile kasikia ninahela anakuja kuniona kila akiwa na shida tu, basi mpaka leo ndio nipo hivi ninabiashara zangu na mzee wangu.

Najuwa mnaopitia humu ni wazazi, matatizo yenu ya ndoa yasiwafikie mpaka watoto kwani inamdhara makubwa sana, na unapoamua kuzaa uwe kabisa na uhakika utampenda na kumtunza mwanao.

xxxxxxxxxxxx

Reactions:

5 comments:

 1. jamani kwa kweli kisa hiki kimeniumiza sana kama mwanamke na haswa kama mama wa familia. Nimejiuliza hivi kweli mwanamke unaweza kubeba mimba miezi tisa kwa taabu zote za mimba hadi unazaa mtoto alafu inakuwaje unamchukia???? jamani kweli wkt mwingine wanawake tukiitwa viumbe wa ajabu hata sishangai...... japo sio wote, tunatofautiana sana kwa sababu mm sitegemei kumchukia mwanangu eti kisa baba yake ananinyanyasa au amenitenga,nitahangaika na mwanangu/wanangu kwa hali yeyote ile!!!

  Nampa polesana huyo kaka japo hakutuambia haswa kwann mamayake aliamua kusema maneno ya chuki dhidi yake, na kama ni ugomvi wa kifamilia kwnn amemuhusisha mama pekeyake? na baba pia alitakiwa kulaumiwa.

  ReplyDelete
  Replies
  1. lakini bado hiyo hai-justify yeye kuwa shoga. wangapi wanateseka mitaani na hawafanyi hivyo? kama kibarua japo cha zenge alipata. huyu ni msenge tu na anapenda kulalwa na midume yenziye. limeniudhi!!!

   Delete
 2. kaka, pole sana. natambua wewe pekee ndo unayejua maumivu uliyo nayo ila nakuahidi nitakuombea kila wakati ili upate furaha na amani maishani mwako.

  serikali na jamii kwa kiasi kikubwa hatuna huruma na watu wa aina yako, na wala hatuangalii ni kwa nini mpo hivyo. Nisamehe, ila inabidi nikuulize, umewahi kujaribu kuacha? nauliza hivi kwa sababu kutokana na stori yako sidhani kama unafurahia hali yako. Ningependa tuwe marafiki, my email is u.bandala@aol.com

  Dada P.

  ReplyDelete
 3. Yawezekana mama yake alimzaa mtoto huyo na mwanaume wa nje. Ndiyo maana akamchikia

  ReplyDelete
 4. Mh kaka pole ila hukutakiwa kukubali kufanyiwa hivyo, kwan alishakunulia kila kitu, mm ningeamuakuhama na kwenda hata kwa ndugu yangu, nengemuelezea mwanzo mpaka mwisho then angenipokea tu. ila wazazi jamani tuangalie sana mimba miezi tisa alafu unamtelekeza mtoto wako sio vizuri kwakweli hebu fikilia uchungu ulioupata wakat wakujifungua alfu leo unamkana mwanao mmmmh pole kaka yangu
  Grace wa Kimara

  ReplyDelete