Sunday, February 5, 2012

Dada Rose,

Hivi hii tabia wanaume wanayofanya ya kutupiga sisi wanawake imetokea wapi tena mbona nilikuwa nadhani hii yalikuwa zamani na sasa hamna tena nimeshasikia wanawake wengi wamepigwa na wapenzi wao hata mimi pia ni victim wa kupigwa na mpenzi wangu halafu hata sababu siioni.

Mimi ninampenzi wangu, ambaye MUNGU ametubariki tumezaa mtoto mmoja lakini hatukai pamoja kila mtu anakaa kwao, mapenzi yetu kwakweli ni kama mengine tu yenye raha na wakati mwengine pia tunagombana yani kama mapenzi yalivyo.

Lakini cha kushangaza juzi tumegombana kosa ni lake halafu ananipiga, ilikuwaje tumetoka vizuri tumeenda club mara nikawa nimebanwa haja ndogo kwenda chooni kurudi namkuta mwanamke anampapasa sura na kidevu halafu mwenyewe kaka tuu hana hata wasiwasi, nilivyowaona vile nilihisi kama ganzi mwili mzima.

Nilipomfikia na kumuuliza akaniambia eti malaya tu yule anatafuta bwana, sasa nikamuuliza ndio bwana mwenyewe wewe mbona hujakataa asikushike na unajuwa tupo wote hapa akajifanya ananipotezea kama vile namaindi vitu visivyo na msingi mara nimekaa kidogo akaja tena mwanamke yule na kumnong'oneza nikashikwa na hasira na kumkunja na kupigana na huyo mwanamke ikawa vurugu mpaka tukafukuzwa disco.

Tukiwa njiani ananirudisha nyumbani huku bado nahasira naye na kugombana naye tukafika nyumbani nilichomwambia ni kwamba asijetena kunitafuta na kama ni mwanaye atakapokuwa mkubwa nitampelekea eti kwahasira akanivuta ndani ya gari na kuanza kunipiga yani alinipiga mpaka nikapiga makelele kuomba msamaha maana nilikuwa nazidiwa, mara baba yangu ndio akatoka na ndio huyu mpenzi wangu kuniachia na kuondoka hata hakumsalimia baba.

Kwanzia siku hiyo baba na mama wakasema hawataki kumuona wala kumsikia huyo mwanaume, na yeye wala hakuja kuomba msamaha kwa kunipiga bila kosa wala kuomba wazazi wangu msamaha wa kunipiga japo nimezaa naye lakini simtaki tena maana sasa nafikiria kama uchumba tu hivi ananipiga huko kwenye ndoa si ndio ataniua na nitakuwa sina wa kuniamulizia?

Jamani wanaume mwanamke sio wa kupigwa, mwanamke wa kumpiga na vitu vizuri vya thamani (gold, gari, nguo, viatu, blackberry, na vinginevyo) sio kumpiga kwa ngumi kisa cha kumuharibu mtoto wa watu sura ni nini...unatupwa kule kwenye dustbin


Reactions:

3 comments:

 1. Unapigwa kisa unakuja kusimulia kwenye blogu eti hakuja hata kuomba msamaha wazazi wangu. Yaani wanawake kwa kweli bado sana inabidi mrudi tena shule elimu mliyonayo haiwasaidii. Mtu yeyote akikupiga ni kosa la jinai. Hata wewe ulivyopigana huko club ni kosa la jinai pia siku nyingine usirudie utakuja kukutana na mtu anajua haki zake atakufunga ukanyee debe jela.

  Pili kama ulikuwa hujui huyo uliyeambiwa ni malaya tu ni mke mwenzio. Mwanaume hawezi kureact kama alivyoreact huyo jamaa yako kisa tu umemgombania kwa malaya aliyekuwa anamtongoza. Kama huamini watume watu wakakuulizie huko kama huwa hawamuoni akiondoka nae.

  Tatu mwanaume huyo hana adabu wala woga na amekuonyesha dharau kubwa kuwa wewe si lolote si chochote ndio maana ameweza kukudunda nyumbani kwenu. Siku nyingine atakuvunja mguu mbele ya wazazi wako, kisa umezaa nae! Uamuzi na wako na ukishaoea kuwa abused hutasikia ndewe wala sikio.

  ReplyDelete
 2. polee shoga, mimi binafsi mwanaume wa kunipiga sitaki hata kumsikia nawaona ni wanyanyasaji wa kutupwa and hawana courage ya kuface makosa yao, wao wanaona manguvu yao ndo solution.
  mie nishawahi kua na mtu kama huyo nilimkimbia wala sikutizama nyuma, thou nilikua nampenda kufa, inaoneakana hana adabu kabisa, atakubalije mwanamke tu yoyote amshike hivo tena mwenyewe kamwita malaya?? kwa kweli hiyo ni kukoseana heshima.
  fikiria mwenyewe kama unaweza kuishi na mtu kama huyo, je utaweza vumilia mambo hayo kama hatobadilika.
  ongea na moyo wako mamie, wala usiogope kufanya maamuzi yoyote kwenye maisha lazima uchukue challenge.

  ReplyDelete
 3. yani WE MEN (WOMEN) SHALL NEVER WIN! KHAAAAAAAA! NIMECHUKIAJE?

  ReplyDelete