Wednesday, February 1, 2012

Habari dada Rose,

Wanawake wamekuwa wakilalamika sana kuhusu wame zao kuwatenda, ni kweli kabisa kuna ndoa nyingi ambazo hazina amani na chanzo cha kukosa amani ni sisi wakina baba, lakini leo nakuandikia kwasababu ya ndoa ya rafiki yangu ambaye mke wake ndiyo tatizo la kwao kutokuwa na amani.

Mke wake ni mtu wa kulipiza sana visasi, kuna wakati jamaa kweli alitoka nje ya ndoa na kwa bahati mbaya ama nzuri mkewe akagundua ilikuwa ishu kubwa sana lakini baadaye tunamshukuru MUNGU yule mama akakubali yaishe na kurudiana na mumewe na ungewaona hakuna ambaye angeamini kama walishakuwa na ugomvi mkubwa ambao ungewafanya waachane.

Kumbe yule mwanamke alidhamiria kumlipizia jamaa lile tukio, kuna wakati naye akapata mpenzi nje, wakawa wanafanya kwa siri lakini mapenzi ya nje yakamnogea mkewe ikafika kipindi akashindwa kuyaficha bila kujua hata pale mumewe anapoamua kumtoa mkewe out yule dada humtaarifu mpenzi wake na kumwambia aje hiyo sehemu na yule kaka huja na rafiki yake yule mke wa rafiki yangu..kwahiyo rafiki yangu hujuwa marafiki wameamua kutoka na wapenzi wao bila kujuwa yule rafiki wa mkewe ni galasha na yule jamaa ni mwenziye.

Ikawa hivyo muda mrefu, na mpaka wale wakawa wanakuja kuwatembelea nyumbani yule mwanaume hajui, siku moja ndio balaa lilipotokea wakiwa sehemu moja ya starehe mume akamchukuwa mke wake kwenda kucheza na yule jamaa akamchukuwa rafiki wa mpenzi wake aliyekuja naye (ambao wote tunajuwa mpenzie) kwenda kucheza mara ikapigwa nyimbo ya taratibu jamaa akamkumbatia mwanamke wakaendelea kwa mahaba hapo ndipo kasheshe lilipoanza.

Mara yule mke wa rafiki yangu akawa anaenda kuwakataza wasikumbatiane, sasa tukawa tunashangaa kwa nini akaanza kugombana na shoga yake kwanini anafanya vile mbele yake maneno yakaanza pakwa hapatoshi ndipo yule rafiki yake akaamua kuropoka ukweli.

Jamani pale palikuwa hapatoshi ngumi zilipigwa wale wanaume, mwanamke naye mumewe akampigia yule dada kwa aibu akakimbia na mpaka sasa ni wiki hajarudi nyumbani, mumewe wala hajamtafuta ndugu wanashangaa kumuona kijana peke yake akiulizwa kulikoni anamtukana tu mkewe sasa hatujui kitakachoendelea kwao ni nini kwani jamaa bado anamsaka yule hawara wa mkewe amfundishe adabu.

Nimetoa hii mada ili kwanza kuwataka wame kuwa makini na marafiki wa wake zao tujifunze kusoma mazingira na pili kwamba wanawake hata ukiamua kutoka nje ya ndoa yako (kitu ambacho sikushauri) kuwa makini na muheshimu mumeo usimdharilishe kama yule jamaa alivyokuwa anadharaulika muda wote huo.

Baba D....


Reactions:

1 comments:

  1. mimi siamini hata siku moja kutoka nje ya ndoa yangu ndo itakufa uwe mwenye furaha, ni bora hata ukaamua kuachana na huyo mtu na ujianzie maisha yako mwenyewe, ukisema utoke nje ya ndo unajitesa bila sababu, ndio asubuhi unaenda huko nje kwa kidumu wako,jioni unarudi kwako kwa huyo mwenza ambae cjui "humtaki" cjui unaemkomoa au kumlipizia kisasi yaani hata haielweki, sasa hapo umefanya nn, si bado unarudi kwenye maudhi yale yale, bora muachane kila mtu ashike njia yake, lakini kusema utoke nje ya ndoa ni una jitorment bila sababu.

    ReplyDelete