Tuesday, January 31, 2012

HELLO VALENTINE...

ndugu zangu valentine ndio hiyo inakaribia....

Lakini je tukiwa tunikaribisha valentine's day ama siku ya wapendanao wewe mwenzangu unajuwa vizuri maana yake ama unachofikiria ni zawadi mpenzi wako atakayokuletea? maana ya hii siku kweli unaijuwa na kuitendea haki?

Wewe kama mume/mke najuwa kama kweli mnapendana na ndio maana mpaka mkaamua kuoana lakini je siku hii unamtendea haki mwenza wako maana wengine wanaishi pamoja lakini walishapeana red card ya ndoa siku nyingi sana.

Jamani thumuni ya kuandika hii leo ni kusema valentine's day ni siku ya wewe kumuonyesha mtu uliyemchagua kwamba unampenda, unamthamini, na kumshukuru kuwepo katika maisha yako ni nani jibu unalo wewe.

Siku hii tuache unafki na nyie msioweza kutulia na wake/wame zenu hebu muheshimu mwenzako japo siku hiyo sio ndio unaenda kwa hicho kidumu chako siku nzima unategemea mwenzio atapewa upendo na nani, jamani hata umfikirie mwenzako kwa kumnunulia hata pipi.

Unaweza ukawa huna mpenzi na kuamua kusherekea hii valentine na wazazi wako, watoto wako, ama rafiki zako..cha muhimu ufurahie na uonyeshe upendo wa ukweli kwao.


Reactions:

2 comments:

  1. Dalal Rose mm napenda kuongezea kuwa pia tupende kujifunza kitu kimoja, akina mam/akina baba tunatabia yakusema aaaa kwani vallentine ni nn hapana hiyo ni siku ya wapendanao si lazima awe mumeo au mkeo kuna watu mbalimbali wakuwapenda hebu jaribu siku hiyo kuonyesha upendo huo kwa yule unayedhani unampenda kwa dhati kabisa, wakina mama msisahau kumpa zawadi mumeo na akina baba pia, vallentine ni siku yakukaa na umpendae nakuongelea mambo mbalimbali yaliyotokea nyuma yaliyowakwaza nyote ni sikuyakusameheana
    grace kimara

    ReplyDelete
  2. yes, ni valentine jamani, japo tunapenda kujisemesha ooh kwangu mie kila siku ni valentine, ndio kila siku ni valentine lakini hii moja ifanye iwe special, apate kuikumbuka mwaka mzima mpaka ile nyingine ikija. mwanamke ubunifu na hii ifanye iwe moja wapo, mpaka mwenza wako anakua anaitamani ije maana anajua kaandaliwa vitu zaidi anavopewa kila siku.

    ReplyDelete