Thursday, January 5, 2012

Samahani dada natumaini wewe ni mzima, mimi ni kijana wa makamo sijaoa na kwasasa sina mchumba ila kipindi cha nyumba nilikuwa na mwanamke ambaye nilibahatika kupata naye mtoto mmoja japo huyu mwanamke tuliachana kwa vurugu na mwanaume mwenzangu akidai yule ni mwanamke wake na yule ni mtoto wake hapo kabla mtoto hajazaliwa.

Baada ya mtoto kuzaliwa nilikaa kama miezi mitano ndipo nikaamua kwenda kumuangalia kwamimi nadhani yule ni mtoto wangu maana naona kuna vitu amefanana na mimi au hata wazazi wangu, baada ya sokomoko lote hilo la kuvutana kuhusu mtoto niliwaarifu wazazi wangu wakaniambia niachane tu na huyo binti na kama ni mtoto basi atakuja tu kunitafuta baba yake na nilipoawaambia kwamba nimeshaenda kumuona na ninajuwa ni mtoto wangu hawakuwa kabisa upande wangu huku wakiniambia inawezekana sio wako maana siuligombana na kijana mwengine kuhusu huyo mtoto????

Mwanamke yule amenihakikishia kwamba mtoto ni wangu na nimeanza kupeleka mahitaji ya mtoto tokea kipindi hicho mpaka sasa mtoto anamiaka miwili lakini kinachoniumiza kichwa ni kwamba wazazi wangu hawamtaki wanasema sio mtoto wangu na ninashindwa hata kumpeleka kuona ndugu zangu kwani hawamtaki kabisa.

naombeni ushauri mwenzenu nifanye nini? mwanangu yule namtaka na sitaki kuwakosea wazazi wangu.

Reactions:

3 comments:

  1. mbona jb rahc! mchukue mtoto mkafanye kpmo cha DNA, majb yakitoka km n wako wapelekee wazazi wako wamtambue kuwa n mwanao.

    ReplyDelete
  2. Wewe na mwanaume mwenzio wote mnamlea huyo mtoto, mwenzio anachukua matumizi kote kote. Fata ushauri wa kwanza wa kufanya DNA ili ujue ukweli, sio eti nimefanana nae masikio sijui vidole vya miguu, karne hii bado mnafananisha vidole, sura na masikio? Kafanye DNA wewe ujue mbivu na mbichi.

    ReplyDelete
  3. DNA ndiyo jibu sahihi. Kufanana siyo issue, mbona watu wengi hufanana japo siyo ndugu? Kaka achana na huyo mwanamke pamoja na huyo mtoto siyo wako! Wazazi wako wanayo akili timamu na wanajua mengi, hivyo wasikilize na utekeleza maoni/ushauri wao. Usidhani hawapendi kumuona mjukuu wao. Wanaona umeshaingizwa mjini na huyo mwanamke. tafuta mwanamke mwingine huyo hakufai kabisa. Je, huyo mwanamume mwingine naye akiwa ngangari kuwa huyo ni mwanaye na athibitishe anavyofanana na mwanaye labda kucha, nywele, miguu na pua,wewe utasemaje? Kama viungo vyako viko sawa na vinafanya kazi tafuta mwanamke mwaminifu na siyo mapepe kama huyo! Tangaza nia watakuja wengi na utachagua umpendaye.

    ReplyDelete