Tuesday, January 3, 2012

KIZAAAAAA ZAAAAAAAAAA

Dada Rose, kweli nimeamini mkuki kwa nguruwe kwa binadamu mchungu mimi kabla sijampata mpenzi wangu nilye naye nilishazaa mtoto na wakati anataka kuwa nami wala sikumficha na akakubali yote tukawa wapenzi na tulivyoanza kuwa wapenzi bado alikuwa anaishi nyumbani kwa wazazi wake.

Nikawa naenda kwao vizuri kumsalimia wazazi wake wakanikubali pamoja na ndugu zake siku zikaenda siku moja wazazi wake akwaambia ukweli kuhusu mimi kuwa na mtoto.

Kwakweli hawakulipokea kwa uzuri hili jambo na kumwambia yule kaka aachane na mimi, lakini kwa mapenzi kwangu hakuweza kuniacha, basi nikawa naandamwa nikienda kwao na maneno kibao haswa kutoka kwa mama yake na dada zake, kwamba mimi mtu mzima namfwata nini mtoto mdogo kisa tu nimezaa wakati kiumri tupo sawa na maneno mengine mengi.

Mpenzi wangu siku akachoka na kuniambia nitafute nyumba ili ahame kwao tukae wote, basi nikafanya hivyo kijana akalipa kodi akaja na nguo tu tukaanza kunua vitu wenyewe mpaka nyumba ikapendeza na wakati huu nilipohamia kwake mwanangu yeye yupo kwa wazazi wa baba yake.

Masikini kumbe bila kujuwa nikaona maisha si ndio haya nilimpenda sana mpenzi wangu na kumuamini asilimia mia na kumi kwamba kila mtu kafika kwa mwenzake kumbe nilikuwa najidanganya, wakati tumeshatulia kama mke na mume (kwakuishi tu pamoja) kumbe huyu mwanaume akaanza kutokuwa mwaminifu akawa na mwanamke nje na kwa bahati mbaya ama nzuri akapata mimba!!!!!!!!!!!

yule mwanamke akamwambia mpenzi wangu wala hakuikataa lakini akamweleza hataweza kuwa naye kwani anamchumba(ambaye ni mimi) anataka kunioa kwahiyo atatunza tu mtoto na wakati wote huu huyu dada akiwa mjamzito alishaenda mpaka kwa wakwe zangu wakawa wanamuhudumia wakisubiri mtoto azaliwe na kweli amefanana sana na mpenzi wangu.

wakwe zangu wakamuelekeza huyu hawara na wazazi wake kwangu ili waje kuonana na baba mtoto aanze kumpa matumizi, siku hiyo nakumbuka nilikuwa peke yangu nyumbani nimemaliza kufanya usafi nikaamua kujipumzisha kwenye sofa naangalia movie nikasikia hodi kwenda kufungua mlango nakutana na mdada kabeba mtoto, pamoja na mmama mtu mzima na dada wa yule msichana wakaniuliza hapa ndio kwa bwana...... nikawaambia ndio karibuni wakaingia ndani.

Walipoketi wakaniuliza..... yupo nikawaambia hayupo katoka atachelewa kurudi wakaniuliza kwani wewe nani yake nikawaambia mimi mke wake, yaani ghafla nyuso zao zikabadilika yani kwa mshangao wakawa wananong'onezana sijui nini wanajua wenyewe. nikawauliza kwani nyie kina nani wakaniambia huyu mwenye mtoto mwanamke wake na huyo mtoto wake(yaani baada kusikia hayo maneno nikasikia kama kisu kimenikata tumbo) na miye mama wake hawa na huyu dada yake!!!!!!!!!

Wakaaga wakasema akija nimwambie kwanini haleti hela ya matumizi na baada ya siku mbili wataenda kwa mjumbe, wakaondoka nikaishiwa nguvu roho ikaniuma, alipokuja tu mpenzi wangu nilisikia kama kumbonda japo ndio nami nina mtoto lakini wake sikumkuta naye amempata wakati tupo pamoja tayari kama angetaka siangenizalisha?

Majibu aliyonipa ndio yamenichanganya kabisa kwamba alifanya hivyo ili wazazi wangu wasiendelee kuninyanyasa kuwa na mtoto nje, ili wote tuwe sawa tukiamua kuzaa tunazaa tu mmoja ama wawili wetu sote..kwa upande mwengine nilifurahi kwani manyanyaso ya wazazi na ndugu yangeisha lakini kwanini alinisaliti hata kama kwa mema halafu bila condom na haya magonjwa!!!!!

Wazazi wake na ndugu zake wanajipanga kuja kwangu kuniomba msamaha na kumuombea mtoto wao msamaha, wameshapeleka barua ya uchumba kwetu na maandalizi ya ndoa yanataka kuanza lakini moyoni bado ninauchungu na bado nampenda mpenzi wangu sana na ninataka anioe.. kwasasa ni MUNGU tu tunayemtegemea kutuongoza maana mambo ni magumu..

Nioombeeni jamani maana nipo kwenye wakati mgumu.


Reactions:

2 comments:

  1. naomba nikkuite mke mtarajiwa,kwa kuwa mume wako amakwambia ukweli na tayari wakwe zako wamekuomba msamaha,unatakiwa kusamehe kabisa na usiwe usiwe na kinyongo,amua kusamehe kabisa na mpende mmeo kama ilivyokuwa mwanzo mnaanza hadi mkashawishika kwenda kuishi pamoja kwa kuepuka maneno ya wakwe zako.

    na kikubwa ni kumshirikisha mungu katika mapenzi yenu ili aweze isimamia na kwa kufanya hilo utaenjoy maisha ya ndoa milele.

    ReplyDelete
  2. Kama kweli unampenda, msamehe na muendelee na maisha.Ukweli ndo huo alifanya hivyo ili kulinda penzi lenu. Kwhiyo shosti we jisort tu na kaa mkao wa kuwa Mrs.

    ReplyDelete