Thursday, January 5, 2012

HII NI KWA WA BABA...

Jamani leo natoa hili dukuduku kwa wababa, unajuwa wewe umeoa na MUNGU kawabariki kuwa na watoto, kwavile wewe na mkeo wote mnafanya kazi mmebahatika kuwa na uwezo wa kuweka msichana wa kazi, tunajuwa siku hizi wasichana wa kazi ndio kilio cha kila mama aliye naye kwa jinsi wanavyosumbua, halafu wewe baba mkeo unasikia mara kwa mara anamgombeza msichana wa kazi kwa kutokufanya kazi vizuri na mara wakati mwengine utasikia mkeo anamtishia msichana wa kazi baba akija nitakusemea halafu badala ya wewe hata kuongea na dada aelewe kama hilo ni tatizo unakaa kimya haipendezi hata wewe baba unajukumu kwenye nyumba yako.

Nimesikia hiki kilio kwa wamama wengi wenye wame na wasichana wa kazi, baba hebu na wewe mara moja hata ndani ya miezi miwili msaidie mkeo asione kwasababu ni mama majuku yote ya kuchosha ni yake wewe ukija kilakitu ukikute sawa.

Reactions:

1 comments:

  1. na kweli je, cku zte sie wanawake 2naonekana na midomo humu majumbani. Tena akina baba wengine utasikia wanasema ahh we nae ushaanza makelele na huyo binti. Cku moja moja si mbaya na we baba ukaingilia kidogo pale unapoona panastahili. Kuna mahousgal wanawapiga hta hao mama wenye nyumba sa nyingne ishatokea, na wanajua mababa hta hawatiliagi maanani kbsa.

    ReplyDelete